Friday, July 20, 2012

Shughuli ya kutafuta maiti Zanzibar


                                                                              Ramani


                                              Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya M.  Kikwete

Shughuli ya kutafuta maiti kwenye ajali ya meli iliyozama nchini Zanzibar ilianza leo mapema huku watu miamoja wakiwa bado hawajapatikana baada meli iliyokuwa inaelekea kisiwani Zanziabr kuzama eneo la Chumbe.


                                                 Meli ya Star Gate ikizama

Meli hiyo ilitoka Dar Es Salam jana mcahan kuelekea kisiwani ikiwa imebeba watu miambili tisini.Hadi kufikia sasa maiti 31 wamepatikana huku watu zaidi ya 150 wakiokolewa.
Msemaji wa polisi , Zanzibar aliambia shirika la habari la AFP kuwa kwa sasa kuna hofu ya kutopatikana manusura wowote waliokuwa katika meli hiyo ya MV Skagit
"shughuli ya kuwatafuta manusura na maiti inaendelea lakini kwa sasa ni vigumu kwa kweli kupata manusura." alinukuliwa akisema msemamji huyo wa polisi.
Siku tatu za maombolezo
Manusura walisema kuwa walihofia baadhi ya wasafiri wa meli hiyo walikwama katika meli ilipobiruka na kuanza kuzama kwa sababu ya upepo mkali.
Ali Mohamed Shein, rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa.Meli hiyo iliondoka Dar es Salaam saa sita mchana kwa saa za Afrika Mashariki hapo jana ikiwa inelekea kisiwani Zanzibar.


                                                                 Dr Shein Rais wa Zanzibar

Hamza Kabelwa, afisaa mkuu mtendaji katika idara ya hali ya hewa nchini Tranzania, aliambia BBC kuwa onyo lilitolewa kuhusu hali mbaya ya hewa na hivyo vyombo vya majini havikupaswa kufanya safari zozote.
Waziri wa usafiri wa Zanzibar aliambia waandishi wa habari kuwa watalii wawili kutoka Ulaya ni miongoni mwa waliofariki.Shughuli za uokozi zilisitishwa jana jioni kwa sababu ya dhoruba kali ya upepo.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salama,Hassan Mhelela aliambia BBC kuwa jamaa wengi wa watu waliokuwa kwenye meli hiyo walikuwa na wasiwasi na walikuwa wanajipanga kutumia ndege kwenda Zanzibar kutafuta jamaa zao.


Kivukio hicho kati ya Dar es Salaam na Zanzibar hutumiwa sana na wenyeji pamoja na watalii
Mwezi Septemba mwaka jana, takriban watu 200 walifariki baada ya meli iliyokuwa imejaza watu 800 pamoja na mizigo, kuzama huko Zanzibar.


No comments:

Post a Comment