Tuesday, July 10, 2012

Wabunge Wa Wenzetu Hewani


Mambo hayo! Wakati wabunge watanzania wao wameamua kuzogoa mjengoni na mahali hapo patukufu kufananishwa na soko la kariakoo, taifa la Jordan limeingia doa laa ajabu lisilotoka hata kwa jik na kusababisha waingie katika kitabu cha Guiness book of records!! Y? twende sawa sasa.
Mbunge Mohamed Shawabka anashikiliwa na wana usalama wa Jordani kwa jaribio la kutaka kumdhuru mbunge mwenziwe kwa bastola ndogo wakati wakiwa katika mahojiano ya live, katika kituo cha Television cha taifa la Jordan.
Mohamed Shawabka katikati ya kipindi hicho cha TALK SHOW alimtolea bastola bwana Mansour seif edine murad ambaye ni mdau wa masuala ya kisiasa baada ya kuambiwa kwamba yeye ni kibaraka wa rais  BASHAR AL ASSAD wa nchini SYRIA.
Hata hivyo kabla hajatoa bastola hiyo Bwana SHAWABKA alimrushia kiatu mpinzani  wake ambacho kilimkosa na kiatu hicho kikatua kwa mtangazazji wa talk show hiyo MOHAMED HABASHNA ambaye pamoja na  kuamulia ugomvi huo bila ya mafanikio yoyote akaona isiwe taabu akafunga mazungumzo hayo iliyokua ikitizamwa,na mandhari yake yalikua sege mnege na hakuna aliyejeruhiwa katika sakata hilo. ona hapo chini.





No comments:

Post a Comment