Wednesday, July 11, 2012

Kenge wa kipekee




  kakupa bonge ya swagger!huyu ni kenge!anatokea Mwanza tu hapo! Mungu ana mambo! dah kampambaje?kwa jamii hii mwanaume ndo huwa amepambwa namna hii, naamini nia ni kuvutia mademu.na hata alipokua akipigwa picha alipose kama spiderman mwenyewe!Mungu kaumba sifa na utukufu ni kwako baba Muumba.

kenge  huyo kutoka Mwanza aliyepelekwa katika eneo la Agama, mwenye asili  Africa na kwa kawaida huishi katika makundi na dume moja ndo huongoza kundi hilo na kwa asili hua ana rangi kama huyu!
Mpiga picha wa picha hiiCassio Lopes   alikua na raha isiyo elezeka na kusema huyo ni mmoja wa wanyama ambaye hajawahi kumwona tangu amezaliwa na mnyama aliyepakwa rangi nzuri namna hiyo! Na anafanana mno na spiderman kuanzia kifuani,mabega na miguu na anaonekana kama amevaa suti ya spiderman wakati alipokua akitambaa kwenye mwamba




                                   Kuna kufanana flan na spider man siyo? tazama kwa makini.




huyo kaka Cassio Lopes  ndiye aliyepiga picha hiyo, alikua Kenya kwa holiday! akiwa na mkewe  Alessandra

Picha hiyo ya Kenge ilipigwa wakati mpiga picha huyu  Cassio Lopes alipokua katika  Masai Mara National Park nchini Kenya akiwa na mkewe Alessandra.Cassio ana umri wa miaka 38 raia wa Sao Paulo, Brazil,na akiwa katika katika kazi zake za upigaji picha ,mchana mmoja waliamua kupumzika karibu na mto  Rongai.kulikua na ukame wakati huo, na tuliambiwa kua wakati wa asubuhi chui huonekana karibu ya hapo hivyo, hivyo tukaamua kupoteza muda ili kuwashuhudia chui!wakichomoza mtoni.
Baada ya muda mrefu bila kuwaona chui ,tukaanza kuangalia vitu vingine na mkewe ndiye aliyekua wa kwanza kumwona kenge huyo akiota jua juu ya mwamba jirani na mto Rongai.
Hii ni mara yetu ya kwanza kuona mnyama kama huyo japokua tumekwisha wahi kuja Africa mara kadhaa huko nyuma ,tulichanganyikiwa kwa rangi nzuri zakenge!na kitu kibaya zaidi mara tu baada ya kuona mwanga wa flash ya kamera  kenge huyo aliishia zake  miambani.
Na Cassio anamuelezea kienge huyo kwa tabia kwamba ni mwenye aibu mno kuliko hata Spiderman  mwenyewe na Cassio anaamini kua kenge  huyo aliwaletea  bahati kwani baada ya kuishia miambani ndipo  walianza kuwaona chui wakijitokeza! Ambao lilikua lengo letu hapo Mwanzo!

kwa kawaida huonekana hivi!


huyu amejitwalia rangi za Leopard!


walichokua wanakitafuta!

No comments:

Post a Comment