Wednesday, July 18, 2012

Drake Anamiliki Mjengo Mpya Na Hii ni Sehemu


Rapper mwenye hit zinazouza mbaya, ni kama anauishi ule usemi usemao unaishi mara moja tu! Ameangusha dola milioni 8 kwa kununua bangaloo huko Los Angeles,na kufanya ndoto zake kua kweli.





Mjengo huo wa ajabu wa Drake una futi 7,444  na uko katika heka tatu katika vilima vilivyojificha imemgharimu kama dola milioni 7.7, na mjengo huo una kila kitu ndani yake  na unaendana na gharama yake, ndani kuna mabafu kama tisa  ,vyumba vya kulala saba kuna home theatre,kiwanja cha tennesi na volleyball na kuna pool kali mno! Kama haitoshi! Drake anamiliki maporomoko ya maji, kuna sehemu ya pool ina grotto na baa ya majimaji


                                                    bar! yenye kila aina ya wines!!!!!!

Kama uonavyo si rahisi kuamini kijana wa miaka 25 tu kumiliki Mansion kama hiyo na kuiita nyumbani, lakini ni poa! Kilele cha mafanikio.

                                          Water falls pool  anayomiliki Drake!


Drake anajua kula na wakati, Mansion hiyo mnamo mwaka 2009 ilikua inagharimu  kiasi cha dola 27 milioni, na baada ya bei kushuka hadi dola milioni 9.95 na kupungua tena naye akamudu kuinunua akahamia!





        ukitoka katika poll ya maporomoko ya maji unafuata mkondo unaokuleta katika grotto.


Kwa sasa katika vilima hivyo vilivyofichika nyumba zake si za rahisi huanzia dola 1.2 hadi dola 13 milioni na ma celeb ambao hununua,kuuza,kupangisha wamo akina Britney Spears, John Mayer, Melissa Etheridge, Lisa Marie Presley, Ozzy and Sharon Osbourne,na  the Kardashian-Jenner ndo majirani wa Drake!


                                                                    Theatre ya Drake

No comments:

Post a Comment