Ngadu na mamba! anamtupiamoooo!!!
Cheki nyoka alivyotanua mdomo kama mkono wa binaadamu, ndege kajikunyata zake! akija kutahamaki , kajaa mdomoni mwa nyoka huyo! hapo hatoki kwenye kumi na nane za nyoka.
chura akiwa amedakwa na nyoka eneo la mdomoni! na chura kwa ujasiri mkubwa, japo dakika za majeruhi kamshika nyoka shingoni! kwa vyovyote nyoka atashinda kwani atakua amesha muachia sumu! na hivyo atammeza kiulainiiiiiii.
Chura hana manusura hapo, kwani amebanwa kati kati ya mawe na kama uonavyo anashindwa hata kufurukuta! amesha vimba mwili na macho kumtoka, mwishowe ni kifo.
Papa akijiandaa kumla simbi! japokua avumaye baharini ni papa lakini wengine wapo,ingawa hawana msuli kama wake.
Hebu fikiria sekunde chache kabla ya kifo chako, eh naamini humjui adui atakaye yachukua maisha yako kiukweli kabisa, na hapo Mungu aliweka siri kubwa sana juu ya sekunde chache kabla.
No comments:
Post a Comment