Friday, April 5, 2013
ANGA ACHANA NAYO KABISAAAA! KIBOKO
Huu ni muonekano wa ndani ya ndege! nikiingia huwa naanza kusali kabisaaa! ila inasemekana ndo usafiri makini na salama kuliko mwingine wowote, ila hitilafu ikitokea, hamna rangi utaacha ona!
Angani huwa namshangaa Mungu sana! yaani watu waliamua kutengeneza chombo cha kupaa uende eneo lingine! mwanzoni kwangu ilikua mtihani mkubwa kupaa, but now! uhuuu rahaje?
Hapa mimi huumwa mawingu mazito? ha kingine wakisha ona hivyo wanatupitisha baharini na hivi sijui kuogelea! kwi kwi kwi naumwa kabisaaaaaa!
Huwa sipendi anga liwe na mawingu! kwani huwa yanazingua mno na kuwapa taabu marubani na kuniweka mimi abiria mashakani! dah!
BUT kukitulia, huwa naajabia na kufurahia muonekano wa juu mawinguni!
sio kwenye basi tu! hata kwenye ndege huwa napenda kukaa dirishani, nione vinavyoonekana kwa chini, ila umbali ukiwa mrefu huwa siangalii chini. hahahaha hatareee, check view hiyo!
Rock City kwa ukaribu kiduchuu, nyumba kwa mbali kama takataka! haha jamani! ah MWANZAAAAA! NITARUDI TENA.
Unapokarinia kutua! hapo roho kidoogo inapoa kwamba tumefika, ila shughuli wakati wa kutua kwangu ni taabu kubwa
Ziwa Victoria lenye samaki watamu nnao wapenda?! kwa ladha na minofu yake.'
Mwanza airport huwa inanifurahisha sana! ki muonekano! ila mabadiliko yaja, wacha tusubiri.
Watu wengine huishi katika miamba na mawe makubwa Rockcity! na wengine huwa na uthubutu wa kukaa visiwani kama hapo uonavyo! Mwanza ! Mwanza! hua inanifanya nimtukuze Mungu sana! kwa ulivyo Mji huo! sitasita kuusifu mji wowote wenye kuonesha wazi kazi ya Mungu mwenye Enzi! asanteh!!!
Nadhani yatosha! ila nitarudi kufanya kazi tena Mwanza yako mengi ya kujifunza!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment