Friday, April 26, 2013

UJAUZITO MBELE NI FAHARI


Kim kardashian.

Kwetu sisi hapa Tanzania kutokana na mila na desturi huwe kumkuta mwanamke anaanika tumbo ama ujauzito wake nje ,Na hata kama mwanamke huyo akiwa mjamzito akiwa kaolewa, kwake ni aibu watu wakijua? na ukijua ukamwambia we una mimba? atakuchukia na kukununia muda wote wa mimba mpaka mtoto!

Kisirani cha mimba bado sijakipatia picha! ni vijitabia vya ajabu ajabu sana, tena vya mpito lakini ni kiboko! sasa wenzetu huko mbele wao huona fahari kupata ujauzito, na maandalizi ya kuubeba huwa yanasemwa mapemaaa! na ikithibitika kua  mwanamke ni mjamzito, yeye mwenyewe atakua wa kwanza kuwatangazia ndugu jamaa na marafiki kua ana tegemea mtoto"shes pregnant"! na asemapo husema kwa raha zote! tofauti na kwetu, mnuno mwanzo mwisho!
 Beyonce yeye alisema wazi mwanzoni kua anatarajia mtoto, na baadaye maneno mengi yalisemwa juu ya ujauzito huo, lakini alipita kwa furaha kwenye kipindi hicho cha mpito, lakini sasa ana raha na bintiye BLUE IVY
BLUE IVY amekua na ni mrembo sasa
Baba bebe toto, mtoto huleta furaha katika familia, ona mtoto amtazamavyo babake kimahaba mpaka raha! wapo wasemao ukitaka kuona mapenzi ya dhati angalia macho ya mtoto, pindi umtendeapo vyema, vinginevyo atakuepuka.
Blue Ivy amekua sasa, na kilo zimeongezeka, hafichwi tena! anajiachia na wazazi wake. check baba anavyo mnyanyua na unaona dhahiri kua mtoto menyu yake safi! afya ni ya kuridhisha.
 Busu la raha!
ALL EYES ON HER! RAHAAAAAAAAA

Kwa wale ambao huwa wananuna, mi hujiuliza, je umelazimishwa? kua na raha, maana kuitwa mama si kitu kidogo, na ni fahari kubwa! haya kwa wewe unaye tarajia mtoto, nakutakia kila la kheri wakati wote wa ujauzito wako.

No comments:

Post a Comment