Thursday, April 18, 2013

MAKAMU WA RAIS DK. BILALI AFUNGUA RASMI MKUTANO WA PAMOJA WA KIMATAIFA WA WATAFITI WANASAYASI AFRIKA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia wadudu wa ugonjwa wa Maralia kwa kwa kutumia Mashine ya Hadubini, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa pamoja wa Kimataifa wa Watafiti wanasayansi wa Afrika, alioufungua  Aprili 16, 2013 jijini Arusha.

 Makamu wa Rais Dkt. Bilal,akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuuwa Mawasiliano wa Kampuni ya Utafiti, Mafunzo na Huduma ya Ifakara Health Institute, David Mbulumi, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika mkutano huo.
 Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na  Dkt Martha Lemnge, baada ya kuwakabidhi tuzo zao jana. Kulia ni Mkurugenzi wa NIMR, Dkt. Mwele Malecela
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal,akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuuwa Mawasiliano wa Kampuni ya Utafiti, Mafunzo na Huduma ya Ifakara Health Institute, David Mbulumi, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika mkutano huo
 Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, pamoja na Mkurugenzi wa NIMR, Dkt. Mwele Malecela wakizindua rasmi awamu ya nne ya Vipaumbele vya Tafiti za Afya kwa mwaka 2013-2018

No comments:

Post a Comment