PIGO LINGINE! Bi Kidude amefariki dunia huko Zanzibar. ingawa mara kadhaa Bi kidude, ambaye amejipatia sifa na umaarufu ndani na nje ya nchi, amekuwa akizushiwa kifo kutokana na kuuguawa muda mrefu....Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha mfagimarigo, lakini wakati wa uhai wake Bi Kidude alikua hajui tarehe halisi alozaliwa,isipokua alichokua akikumbuka ni kwamba alizaliwa wakati fedha aina ya Rupia ikitumika kama fedha, na uhakika mwengine ni kwamba kabla ya vita vikuu vya dunia vya kwanza yeye alikuwako, hivyo inakadiriwa Bi Fatma alikua na miaka zaidi ya mia!
Bi Kidude, alianza shughuli za kuimba akiwa na umri wa miaka 10 tu! nnachojua miye! bibi alijifunza kuimba kutoka kwa Siti Binti Saad, lakini mpaka bibi anakufa, anapinga kua alijifunza kutoka kwake...MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI--AMIN!
No comments:
Post a Comment