Friday, April 26, 2013
MBEZI YA KIMARA YAINGILIWA!
Ni nadra sana kusikia ama kuona malori yakiibiwa mizigo eneo la mbezi kituo cha zamani, lakini alfajiri ya leo lori hili aina ya fuso lilikumbana na viroba vya pumba za mbao barabarani na hivyo kuanguka,thanx God walokuwemo walinusurika ila mmoja wao ameumia mkono.
namba zake ndo hizo na limepinduka kichwa chini,miguu juu, likiwa na creti za nyanya kutoka mikoani kuja dar kwa biashara. katika jiji la Dar-Es-salaam zimepanda bei mno, sasa hujuma kama hii inarudisha maendeleo ya mtu nyuma. na sababu ya kuwekwa viroba hivyo barabrani haijajulikana
Kwa karibu namba za fuso hizo hapo
Yaani hizi ni chache tu zilizookolewa! katika fuso lote hilo!
Kreti nyingi zilivunjika na hivyo kuruhusu nyanya kutapakaa eneo la tukio.
Na hivyo basi iliwalazimu akina kaka hawa kuziokota nyanya zitakazo faa kwenda sokoni.
Hali si hali, kumbuka wakati huu wa saa kumi na moja alfajiri mvua ilikua inanyesha wakati huo na hivyo kusababisha uokotaji wa nyanya hizo kua wa kusuasua.
Hata hivyo akina kaka hawa ambao waligoma kutaja majina yao, walikua wanaendelea na kazi hiyo ya uokoaji nyanya hizo. Kegajo blog inatoa pole kwa aliyeumia,mwenye lori na hata dereva wa fuso hilo kwa fadhaa aloipata wakati wa ajali hiyo. asante. naomba kuwakilisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment