Thursday, April 25, 2013

Zaidi ya watu 80 wapoteza maisha kufuatia kuporomoka kwa Jengo huko Bangladesh


                                                Shughuli ya uokoaji ikiendelea.

Vikosi vya uokoaji vimeripoti kuwa watuzaidi ya 80 wamefariki huko Bangladesh nje kidogo ya jiji la Dhaka baada ya jengo la ghorofa 8 kuporomoka leo asubuhi.



Inasemekana kuwa jengo hilo lilijengwa chini ya viwango hali iliyopelekea nyufa kuonekana toka jana. Baada ya kuona hivyo baadhi ya watu waliomba kuacha kuendelea kufanya kazi lakini walizuiliwa na mabosi wao.

Shughuli za uokoaji zinaendelea na watu wapatao 200 waliokolewa. Jengo hilo lilikua na benki, kiwanda cha nguo pamoja na maduka kadhaa.

No comments:

Post a Comment