Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi Haji Makame, akisaini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili kuhudhuria misa maalum ya kumwombea aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini, Mh Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi Haji Makame akibadilishana mawazo na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dk Ishaya Samaila Majanbu (kushoto).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule na kulakiwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisubiri kwenda kutia saini kitabu cha maombolezo kabla ya kuanza kwa ibada maalum ukumbini hapo. Kushoto ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisaini kwa huzuni Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini, Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 mei 2014. Kulia ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila wakilia kwa uchugu pamoja na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole wakati wa misa maalum ya kumwombea aliyekuwa balozi wa Malawi nchini Tanzania Mh. Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisalimiana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole. Katikati ni Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila.
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole (mwenye mtandio mweupe) akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania nje ya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga ukiingizwa kwenye ukumbi tayari kuanza kwa ibada maalum na kutoa heshima za mwisho.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga.
Mchungaji akiongoza ibada maalum ya kumwombea marehemu Flossie Gomile Chidyaonga.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bi. Tonia Kandiero (kushoto) akiwa na baadhi ya mabalozi pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania wakati wa ibada maalum ya kumwombea marehemu Flossi Chidyaonga iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Nyuso za simanzi zikiwa zimetawala ukumbini hapo.
Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria ibada msiba wa Balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard K. Membe (Mb) akiwa mwenye huzuni kubwa kwenye misa ya kumwombea marehemu Balozi Flossie Chidyaonga.
Familia ya karibu ya marehemu ikiongozwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini, Mh. Chisiza (kulia).
Huzuni, simanzi na majonzi vilitawala ukumbini hapo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa karibu wa familia ya marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro akitoa mkono wa pole familia ya balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero, akitoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga, akishindwa kujizuia wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mh. Filiberto Sebregondi, akitoa heshima zake za mwisho.
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole, akitoa pole kwa wafiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu,(wa tatu kulia) , Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga (wa pili kulia) wakati wa misa maalum ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
No comments:
Post a Comment