Friday, May 9, 2014

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAPEWA SEMINA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Ningu akifungua mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari juu ya utunzaji wa Mazingira na kuelekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mapema mwezi wa Sita.

 Mwendesha mada wakati wa Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari juu ya masuala ya mazingira Bi. Singlunda akitoa maelezo na mwongozo wa mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
 Mmoja ya Wataalam wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira akifafanua Jambo juu ya Siku ya Mazingira Duniani wakati wa Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari juu ya masuala ya Mazingira
 Bi. Matha Ngolowera Afisa Elimu Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akifafanua Jambo juu ya Tuzo ya Rais Dr. Jakaya Kikwete ya Upandaji wa Miti ambayo hutolewa mara moja kwa mwaka wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
 Bi. Fainahappy Kimambo Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akisisitiza Jambo kuelekea siku ya Mazingira Duniani.
 Injinia Ladslaus Kyaruzi Mhandisi Mwandamizi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akitoa mada juu ya Mabadiliko ya tabia Nchi.
 Baadhi ya wahariri wa vyombo Mbalimbali vya Habari wakiwa katika mkutano wa  Mafunzo ya Masuala ya Mazingira wakati wa kuelekea siku ya Mazingira Duniani mapema mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment