Thursday, May 15, 2014

KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO) ATEMBELEA NCHINI TANZANIA


 
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO),  Bw. Raymond Benjamin (kulia) kwa nchi ya Tanzania. Katibu Mkuu huyo atakuwa nchini Tanzania kwa siku tano ambapo tarehe 16 Mei 2014 atakwenda Zanzibar. Tanzania ni miongoni mwa nchi mbili za Afrika ambazo zimepata bahati ya kutembelewa na Katibu Mkuu huyo.


Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), Bw. Raymond Benjamin (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Uchukuzi, mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tano kuangalia namna ambavyo TCAA inafanya kazi. Kulia kwa Katibu Mkuu huyo ni Waziri wa Uhcukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment