Bingwa mtetezi wa French Open upande wa wanawake Serena Williams ameyaaga mashindano hayo, baada ya kunyamazishwa na Garbine Muguruza wa Uhispania kwa seti 6-2, 6-2.
Hii ni mara ya kwanza
tangu Serena Williams kuanza kucheza mashindano hayo kuondolewa wiki ya kwanza
ya mashindano.Imekuwa pigo kubwa kwani dadake pia,Venus tayari alikuwa
ameshaondolewa kutoka mashindano hayo ambayo yameingia siku ya nne sasa.
Dada hawa,Venus na
Serena wametawala ulimwengu wa Tennis kwa miaka mingi.Venus alishindwa 2-6 6-3
6-4 na M-Slovakia Anna Schmiedlova.
Muguruza, mwenye umri
wa mika 20, alimlemea gwiji huyo nambari moja Tennis ya wanawke aliyeonekana
kufanya makosa madogo madogo lakini yakamgharimu sana.
Serena, Mmarekani
mwenye umri wa miaka 32 amewahi kushinda taji hilo mara 17."Najihisi
vibaya kuyaaga mashindano lakini mambo hayo hutokea wakati mwengine,
ntajitahidi mara tano ya hivi leo wakati ujao' Serena alijiliwaza.
Mashabiki wake
walishangaa kuona amezidiwa nguvu kinyume na kawaida yake,huku mpinzani wake
akibaki mkakamavu na makini.
" Nilisi hakuwa
sawa, na nkaona nna nafasi ya kushinda hapa,inanibidi nicheze vyema ndiyo
nishinde! Amesema Muguruza ambae ameorodheshwa nambari 35 katika ulingo wa
Tenis duniani.
Kwa miaka mingi dada
hao wawili wameweza kutamba katika ulimwengu wa Tenis ya wanawake na Serena
ndie mchezaji pekee mwanamke ambae amewahi kushinda zawadi ya zaidi ya $50
millioni kupitia Tenis.
No comments:
Post a Comment