Michelle Obama alaani
kutekwa nyara wasichana
Mke wa Rais wa Marekani
Michelle Obama amelaani kitendo cha magaidi wa Boko Haram cha kuwateka nyara
wasichana wa shule zaidi ya mia mbili
nchini Nigeria. Katika ujumbe wa kila wiki kwenye radio Michelle Obama amesema yeye na mumewe , sawa
na mamilioni ya watu wengine duniani
kote wameingiwa uchungu na wamefadhaishwa na kitendo cha kutekwa nyara kwa
wasichana karibu mia tatu nchini
Nigeria.
Mama Obama ametoa mwito
kwa Wamarekani wa kuwaombea watoto hao
ili warudi nyumbani salama. Katika ujumbe wake Mama Obama pia amesisitiza
umuhimu wa elimu.
No comments:
Post a Comment