Monday, June 4, 2012

Ajali ya ndege Nigeria 150 watoweka



Ma afisa wa Nigeria wanasema kuwa ndege ya abiria imeanguka kwenye eneo la makaazi mengi, katika mji mkubwa kabisa wa nchi ya Nigeria , Lagos.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema waliona ndege ikigonga jengo na kuwaka moto.Ndege hiyo  ilikuwa imebeba kama mia-moja-na-50. Haijulikani wangapi wamenusurika.
Mkuu wa Idara inayoshughulika na safari za ndege, Harold Denuren, alisema ndege hiyo ilikuwa inatoka Lagos, kusini mwa Nigeria, kuelekea mji mkuu Abuja, kaskazini mwa nchi ndege  hiyo ni ya kampuni binafsi ya Dana Air
Ndege hio ilianguka katika eneo lililo nje kidogo mwa uwanja wa ndege.Taarifa ilisema kua wataalamu wa dharura walikua njiani kufika mahali pa tukio.
Habari zinasema kua hali ya hewa ilikua shwari kukiwa na jua bila sababu ya kusababisha hitilafu.
Nigeria kama Mataifa mengi ya Kiafrika ina rekodi mbovu ya usalama wa safari za anga, ingawa juhudi kiasi zimefanywa katika kuboresha hali hio tangu kipindi cha janga la ajali za ndege mnamo mwaka 2005

.Malkia ahitimisha sherehe za miaka 60


Zaidi ya watu milioni moja waliohimili mvua kali wameshuhudia msafara wa Malkia wa takriban mashua 1,000 wakati wa kuadhimisha miaka 60 ya utawala wake kupitia mto Thames.


Mashua ya Malkia ilikua katikati ya msafara wa mashua za aina mbalimbali, zinazotumia nishati ya mvuke, za kupiga kasia, mashua za kifahari, kayak na mjengo wa Kichina maarufu kama Dragon Shughuli hii ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya utawala wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza.
Takriban watu 10,000 walishiriki tafrija ya mitaani huko Greenwich, mojapo ya vitongoji vya jiji la London ikiwa ni mojapo ya tafrija nyingi zilizofanyika kote nchini Uingereza kuadhimisha miaka 60 ya utawala wa Malkia.


Sherehe ilipambwa vilivyo na hao uwaonao, Cathy na mumewe, malkia na mumewe pamoja na Pippa.


Shughuli ya mtoni Thames ilianza rasmi kwa kengele za miaka 60 ya utawala ilipotimu saa nane na dakika 40 saa za Uingereza na zilipangwa kumalizika kwa mashua ya mwisho kuvuka daraja la Tower baada ya safari iliyoanzia kwenye daraja la Albert magharibi mwa mji.
Malkia akivalia kofia nyeupe na koti yenye rangi ya fedha iliyochanganya nyeupe iliyoshonwa na Angela Kelly, alipelekwa kwenye mashua mwanzoni mwa safari kuzindua mashua ya anasa Royal Yacht Britannia na baada ya kusalimiwa kwa wimbo wa Taifa ulioimbwa na ummati wa watu waliokuja kushuhudia sherehe.



Wakati wote Malkia alisindikizwa na wana wa Ufalme wakuu, akiwemo Duke wa Edinburgh(Mumewe) pamoja na Duke na Duchess wa Cambridge, kwenye mashua yao, iliyopambwa mauwa 10,000 kutoka mashamba ya makaazi ya Kifalme.





                                                    Maua yalikua ya kumwaga

Hadi watu 20,000 walikisiwa kua kwenye mashua zilizosafiri leo kwa mwendo wa kasi ndogo ya bahari ya maili nne na nusu kwa kila saa. Wakati wote huo kizuizi cha Mto Thames kilibanwa ili kupunguza kasi ya maji ya Mto.
Shangwe na makofi yalipigwa kila sehemu mashua ya Kifalme ilipoonekana. Baada ya siku yenye kivuli ilimiminika mvua kali lakini haikuonekana kuvunja nyoyo za watu waliofurahia siku hiyo.


shughuli ilkua pevu.




Saturday, June 2, 2012

Maadhimisho ya Miaka 60 ya kua Malkia


QUEEN ELIZABETH


Kuanzia leo waingereza wanavaa nguo nyekundu,blue na nyeupe na beji flani hivi kuadhimisha miaka 60 tangu kutawazwa kua malkia wa uingereza Queen Elizabeth,kesho kutakua maadhimisho makubwa   sana huko Uingereza japokua yapata mwezi sasa sherehe mbalimbali zilikua zilikua zikifanyika.Mizinga 21 itapigwa na sherehe zitafanywa katika mji wa Edinburgh,na miji mingine.
Meli maalum itambeba Malkia na mumewe Prince Philip ,kupita      West London hadi tower bridge akiwasalim watu akielekea katika viwanja vya West Minister Abey.
Kuna wanajeshi zaidi ya 200 ambao wanakwenda Afghanstan watakula chakula na malkia pamoja na familia zao.Na msaidizi wa malkia  Elizabeth ambaye aliajiriwa na malkia kwa miaka 26 sasa hajalipwa hata senti tano yeye ana furahia tu maadhimisho hayo, bibi huyo  yeye alikua mhariri wa bbc idhaa ya  kiingereza na wanafanana mno na malkia  , yeye kama ilivyo itifaki atafika eneo la tukio kabla ya Malkia, na suala la kutolipwa kwake ni matakwa yake mwenyewe kwa heshima ya Malkia Elizabeth aliamua kujitoa kwa malkia huyo ili kumtumikia tu! Si zaidi ya hilo je wewe unaweza?

  

msaidizi wa malkia Elizabeth

Kwa tabia Queen Elizabeth ni mwenye aibu tele,hajawahi kwenda darasani waalimu waliwafundishi kwenye kasri zao. na hupendelea rangi za blue,green na black, na inasemekana siku za hivi karibuni malkia mwenye aibu nyingi amekua akivaa nguo za kifasheni zaidi na kuzungumza mara kwa mara na Cath mke wa Prince Wiliams jambo ambalo si la kawaida.
queen akiwa mtoto.



rangi aipendayo Blue





Justin Bieber apata mtikisiko wa ubongo





Justin Bieber amepata mtikisiko wa ubongo baada ya kugonga kichwa chake chini tangu may 31 kwenye show yake mjini Paris. Bieber  alieleza kua katikati ya wimbo aliokua akiperfom alikimbilia kwenye ukuta wa kioo nyuma ya jukwaa na alipatwa na baridi kama ya dk 15 alipokua akitoka katika chumba chake cha kuvalia  na madaktari wamethibitisha hilo lakini wamewaondoa wasiwasi mashabiki wake kua hana hatari inayomkabili
Bieber  kwa sasa yuko ziarani ulaya kuifanyia promo album yake ya Believe ambayo inatarajiwa kuzinduliwa june 15.

Friday, June 1, 2012

Tuko Wangapi? Tulizana- TACAIDS





Utafiti  wa viashiria vya Malaria na ukimwi nchini kwa mwaka 2010/2011 unaonesha kua theluthi moja ya wanaume walio oa wamekiri kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja ambapo kwa upande wa wanawake walio olewa asilimia 16 wamo kwenye mahusiano ya aina hiyo.
Mwenyekiti mtendaji wa tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania Dk Fatma Mrisho amesema jijini Dar-es –Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘TUKO WANGAPI,TULIZANA  kua watu walio kwenye kundi hilo wanafikiri kwamba hawako katika hatari ya maambukizi ya magonjwa ya ngono ikiwemo kutokana na kuwa wapenzi wawili au watatu kwa muda mrefu. Dr Geofrey Kiangi ameitaka jamii kuingia katika mapambano ya kupunguza maambukizi mapya ya vvu kwa kujiepusha na mtandao wa wapenzi zaidi ya mmoja






Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Fatma Mrisho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kimataifa ijulikanayo kama ‘Tuko Wangapi?, Tulizana’.
 Dk.Mrisho ambayea likuwa mgezi rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Golden Tulip amesema kwamba kampeni hiyo imelenga kuongeza idadi ya Watanzania wanaojua maana ya mtandao wa ngono, hatari ya kuambukizwa VVU kutokana na kuwa mmoja ya wanamtandao wa kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja

mmoja kati ya wasanii walopamba uzinduzi huo, Dogo Aslay!Naenda kusema kwa mama ,kusemaaah!!!



ah MarcReagan wee unanikosha sana unapoigiza kama demu huwa unauvaa uhusika asilimia mia, uh sema na jamaa basi hapo mko wangapi? lol ghahahhaha.



Jiachie bibie  eh, lakini waringa ushajiuliza ama kumuuliza mko wangapi? hahahh utajuta ukitaka kusikia!!!!



mpaka hapa naamini ushapata jibu kwa namna Marc alivyoonesha uhalisia wa mapenzi kitaa yalivyo na mkorogo wa kutosha! TUKO WANGAPI? TULIZANA!!!!!!!!!!



Faida na Hasara ya Mitandao



Hakuna chenye faida kikakosa hasara! Nazungumzia hii zama ya sayansi na teknolojia,kuna faida ya kuifanya dunia kua katika kijiji kimoja, lakini matumizi yakiwa mabaya hasara yake ni  kuwa na kizazi chenye mkengeuko wa maadili.
Kuna usemi usemao mali bila daftari hupotea bi taarifa! Kama hakuna udhibiti katika mitandao na hasa katika internet cafee basi maadili ya mahalia katika kijiji hicho ni janga la kjiji chote haijalishi rangi ama itikadi za wenyeji waishio katika globalaisation! Ah
Tutoke kijijini humo kidogo! Turudi nyumbani Tanzania  tumewahi kusikia kelele wanazopigiwa wamiliki wa migahawa yenye mitandao kua wanapaswa kuhakiki mara kwa mara watu wanao pakua taarifa mtandaoni basi iwe ni taarifa tu na sio ngono! Lakini mara kadhaa tumesikia wanafunzi,wanavyuo na kada zote hawaachi kuingia mtandaoni kutafuta pilau na kuzitazama na mwishowe huondoka hapo na mhemko unaoweza kuwafanya wakabaka ama kupata mfadhaiko!
Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 12 amembaka msichana wa miaka 9 na hiyo ni matokeo ya kuangalia picha za ngono mtandaoni,amenusurika kufungwa jela jana na huku wakili wake akiionya jamii ya watoto na vijana walio katika vipindi vya mpito na hata walio komaa kutotazama picha hizo  maana hazina faida kwao zaidi ya kupandwa na pepo wa ngono anayeishia kuwatupa jela.
Kijana huyo kwa sasa ana miaka 14,anaeleza jinsi alivyo mbaka motto wa jirani yao lengo la kijana huyo ni kutaka kujiona amekua baada ya kuona kilichokua kinafanywa mtandaoni, nay eye anatoa ushuhuda kua hakua akifuatiliwa wakati akiwa mtandaoni na hiyo ikamrahisishia kufika alikofika na kutekeleza alichokidai kuji feel mkubwa!


                                                          dogo akiangali ngono mtandaoni.

Kufuatia kitendo hicho magazine ya Daily mail imeanzisha kampeni ya kufunga mambo ya ngono mitandaoni  Sean Templeton, ambaye ni wakili wa motto huyo anaeleza kua vijana wengi wanakua na kivuli cha mtazamo wa  ngono ni nini? Na shughuli nzima ikoje
Hakimu Lady Smith  aliamua kutoa maamuzi magumu na kusema kijana huyo asifungwe jela na badala yake achanganywe na watoto wenziwe na awe chini ya uangalizi
Mbaya zaidi binti aliyebakwa alimueleza mamake kitambo mbele kidogo kua anahisi akam kuna motto tumboni, alipotakiwa kufunguka alieleza kilichofanya na kijana huyo ,polisi waligungua kua binti huyo alikua mwathirika wa kufanyiwa udhalili huo katika bustani za nyumbani kwao kati ya December 1 na January mwaka 2011 ,kijana huyo alithubutu kumdhalilisha binti huyo akiwa katika chumba cha kijana huyo mbele ya rafiki yake.
Alipokua akihojiwa na polisi alionesha mtandao uliomhamasisha, na akahifadhi picha hizo na alijitetea kua ni mfadhaiko na kutaka kuwa mkubwa ndivyo vilivyo msukuma .baada ya maelezo hayo alitengwa mbali na jamii mile kadhaa mwanzoni mwa mwezi huu alionekana akitetemeka baada ya kusomewa mashtaka na kupatikana na kosa moja la ubakaji na udhalilishaji, atakua chini ya uangalizi hadi miaka 18 atakaposhtakiwa.



Lady Smith


Huo ni mfano huko mbele na ni tone la shtaka lililofika kwa pilato, yapo mengi, je Tanzania tunakilinda vipi kizazi chetu kinachopita katika vipindi vya mpito kisipelekwe na mihemko na kutaka kuwa wakubwa? Wangapi wamebakwa katika jamii zetu na wakaa kimya? Wangapi wamedhalilishwa na kuamua kukaa kimya kwa kuogopa endapo wakienda kushtaki watakua dhalili? Nini kifanyike ili kuvunja ukimya, na jamii inusurike na watu wanaokufa na vihoro kwa walichotendewa walipokua wadogo! Tuvunje ukimya, tafakari.

Picha ya Leo


Mungu anajua kuumba na kuumbua jamani! duu! vichwa viwili na midomo mitatu, du chunguza utaona, hivyo si binadamu tu wanaozaliwa wakiwa na viungo vya ziada! hata wanyama! je hali hiyo inaashiria nini?