Saturday, June 2, 2012

Maadhimisho ya Miaka 60 ya kua Malkia


QUEEN ELIZABETH


Kuanzia leo waingereza wanavaa nguo nyekundu,blue na nyeupe na beji flani hivi kuadhimisha miaka 60 tangu kutawazwa kua malkia wa uingereza Queen Elizabeth,kesho kutakua maadhimisho makubwa   sana huko Uingereza japokua yapata mwezi sasa sherehe mbalimbali zilikua zilikua zikifanyika.Mizinga 21 itapigwa na sherehe zitafanywa katika mji wa Edinburgh,na miji mingine.
Meli maalum itambeba Malkia na mumewe Prince Philip ,kupita      West London hadi tower bridge akiwasalim watu akielekea katika viwanja vya West Minister Abey.
Kuna wanajeshi zaidi ya 200 ambao wanakwenda Afghanstan watakula chakula na malkia pamoja na familia zao.Na msaidizi wa malkia  Elizabeth ambaye aliajiriwa na malkia kwa miaka 26 sasa hajalipwa hata senti tano yeye ana furahia tu maadhimisho hayo, bibi huyo  yeye alikua mhariri wa bbc idhaa ya  kiingereza na wanafanana mno na malkia  , yeye kama ilivyo itifaki atafika eneo la tukio kabla ya Malkia, na suala la kutolipwa kwake ni matakwa yake mwenyewe kwa heshima ya Malkia Elizabeth aliamua kujitoa kwa malkia huyo ili kumtumikia tu! Si zaidi ya hilo je wewe unaweza?

  

msaidizi wa malkia Elizabeth

Kwa tabia Queen Elizabeth ni mwenye aibu tele,hajawahi kwenda darasani waalimu waliwafundishi kwenye kasri zao. na hupendelea rangi za blue,green na black, na inasemekana siku za hivi karibuni malkia mwenye aibu nyingi amekua akivaa nguo za kifasheni zaidi na kuzungumza mara kwa mara na Cath mke wa Prince Wiliams jambo ambalo si la kawaida.
queen akiwa mtoto.



rangi aipendayo Blue





No comments:

Post a Comment