Tuesday, June 5, 2012

Mwaka 2012 ni wa Jose Chamilione





Miezi mitatu iliyopita tulipata taarifa kutoka nchini Uganda namna ambavyo mwanamuziki bora  Africa mashariki na wa sita kwa ubora barani Africa Joseph Chamilions amefanikiwa vilivyo tamasha lake la Valu Valu Concert.


matunda ya Album ya Valu Valu

Lakini kwasasa mwanamuziki huyo  aliyepewa cheo cha daktari wa muziki tangu mwezi wa pili mwaka huu gari yake aina ya range rover imewekwa plate namba ya 'DOCTOR'.



Mwanamuziki huyo baba wa watoto 4, ana bahati ya mtende pengine ujio mpya wa mtoto wake wa nne aitwaye Alba SHYNE Mayanjaa  aliye zaliwa katika hospitali ya Nsambya ,  Jose amepata shavu la kwenda kuperfom kwenye viwanja vya   Wembley Stadium  mwezi August mwaka huu  katika ufunguzi wa michuano ya Olimpiki 2012 mjini London.




       Alba SHYNE Mayanjaa Chanzo cha Mafanikio ya Chamilion na zawadi kwa mama.




               mahali ambapo Jose ata perfoam viwanja vyA Wembley

Kwa upande mwingine kutokana na furaha yake hiyo, Jose Chameleone amemnunulia mkewe aitwaye Daniella BMW  x5  wakatia awali alikua akisukuma mkoko aina ya harrierkama zawadi kwa kumpata motto huyo wa kike ,ingawa wana watoto wa kiume wawili Abba na  Alpha Mayanja. Kwake Joseawali alikua ana motto kwa mke wake wa kwanza mtoto huyo anaitwa  Ayla Mayanja.



                            zawadi ya kuleta mtoto Alba SHYNE Mayanjaa 





Daniela atakaye sukuma BMW x5 akiwa ameshika  kinyonga


Mwaka huu wa 2012 kwake Jose unaonekana kuja vizuri na maajabu tele na amekua mwanamuziki bora Africa mashariki
Vilevile amelamba dili ingine kutoka kampuni ya Samsung la kutangaza bidhaa zao akiwemo mwanasoka Didier Drogba.Jose amechaguliwa kuwa balozi wa Sumsung kutokana na umaarufu wake kutoka Africa ya Mashariki.



Didie Drogba


 

                                                 Jose Chamillione

Jose Chamilione alisha saini dili baya kuliko zote alizokwisha kuwahi kusaini kwa mwaka huu mwezi January kwa kampuni ya Telecoms inayomtaka kuwa balozi wao kwa miaka 5, na hakutakiwa kuperfom kwenye matamasha ya makampuni mengine kama hayo na alipotaka kujitoa ati anabanwa wataalamu wa sheria walimwambia hana budi kusubiri miaka 5 ipite ndipo awe huru, alipokaidi akapoteza mamilioni ya  shilingi.

No comments:

Post a Comment