Tuesday, June 5, 2012

Ajali ya ndege yawaua zaidi ya watu 150


Mabaki ya Boeing MD-83


Siku tatu za maombolezo ya kitaifa nchini Nigeria  zimetangazwa kuanzia jana nchini  kufuatia ajali ya ndege ambapo zaidi ya 150 walikufa.
Ndege hiyo aina ya Boeing MD-83 iliangukia eneo moja la kuchapisha karatasi na makaazi mjini Lagos kabla ya kulipuka. Makundi ya wokozi yamekuwa eneo la ajali usiku kucha.
Taarifa zinaeleza kua abiria wote katika ndege hiyo walikufa. Hakuna majeruhi katika eneo la ajali japo haijabainika rasmi ni watu wangapi ambao wamekufa.




Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Dana Air ambayo hutoa huduma zake kati ya mji wa Abuja na Lagos. Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Iju Kaskazini mwa uwanja wa ndege.
Rais Goodluck Jonathan ameamuru kufanyika uchunguzi kamili kubainisha kilichosababisha ajali hiyo.Mwandishi wa BBC Mjini Lagos Will Ross amesema hapo mwezi Mei ndege nyingine inayomilikiwa na kampuni ya Dana Air ilipata hitilafu za mitambo na kulazimika kutua ghafla.



Nigeria kama nchi nyingi Barani Afrika inakumbwa na matatizo ya usalama wa safari za anga.Hata hivyo kumekuwa na juhudi za kuboresha safari za anga tangu kutokea misururu ya ajali za ndege mwaka 2005

No comments:

Post a Comment