Monday, June 11, 2012

R.I.P Bob Makani


Bob katika harakati zake

Kufuatia kifo cha aliyekua Naibu Gavana wa kwanza wa benki kuu ya Tanzania na katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,BOB MAKANI, chama hicho kimesitisha mikutano yake yote iliyokua ikiendelea katika mikoa mbalimbali ya kusini ikiwa ni  pamoja na kushusha Bendera yake nusu mlingoti kwa siku tatu.
Marehemu BOB MAKANI ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA,amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Aghakhan iliyoko hapa jijini Dar-Es-Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa mapafu,na mwili umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chadema, John Mnyika amesema marehemu Makani anatarajiwa kuagwa leo saa sita mchana katika viwanja vya Karimjee, Dar-Es-Salaam na baadaye mwili wake una tarajiwa kusafirishwa kuelekea Mkoani Shinyanga.
Mnyika amesema kutokana na makubaliano na familia ya marehemu, mwili utakapo wasili huko Shinyanga utaagwa kwa mara ingine tena na kasha kuzikwa eneo la Negesi,wilaya ya Kishapu,mkoani humo.


No comments:

Post a Comment