Dj wa kwanza mdada bongo,Fatma Hassan wa hapa mjengoni Clouds Fm, amepewa heshima kubwa ya kuwa dj wa Kwanza wa kike kutoka barani Africa na hasa Africa Mashariki kusugua mashine kwenye shindano la big Brother Africa ‘StarGame’ 2012.
Kupitia ukurasa wake wa Face book,Fetty ameandika kua leo Jumamosi na Jumapili atakua akispin na kuscrach, ndani ya jumba la BBA Stargame,anahitaji umtumie ujumbe ambao utampa playlist yako itakayowapawisha mjengoni humo.
Dj Fetty ambaye kwa muda alikua amepumzika shughuli za udj na kuendelea na utangazaji wa kawaida,ilimlazimu kujifua tena ili kuhakikisha, haangushi maembe kwenye kumiksi nyimbo wakati akipagawisha katika moja na mbili.
Fettylisious alibainisha kua mwaliko wa kuangusha moja moja aliupata mwezi mei mwaka huu na tangu hapo akaingia mazoezini kwenye wheels of stell, kwa kua hiyo ni nafasi kubwa inayohitaji mandalizi ya kutosha.
GO FETTY GO! GO BAYBY! KILA LAKHERI NA UFANYE VYEMA UTUWAKILISHE MJENGONI! MWANAMKE AKIAMUA ANAWEZA!!!!!!
No comments:
Post a Comment