Friday, June 1, 2012

Faida na Hasara ya Mitandao



Hakuna chenye faida kikakosa hasara! Nazungumzia hii zama ya sayansi na teknolojia,kuna faida ya kuifanya dunia kua katika kijiji kimoja, lakini matumizi yakiwa mabaya hasara yake ni  kuwa na kizazi chenye mkengeuko wa maadili.
Kuna usemi usemao mali bila daftari hupotea bi taarifa! Kama hakuna udhibiti katika mitandao na hasa katika internet cafee basi maadili ya mahalia katika kijiji hicho ni janga la kjiji chote haijalishi rangi ama itikadi za wenyeji waishio katika globalaisation! Ah
Tutoke kijijini humo kidogo! Turudi nyumbani Tanzania  tumewahi kusikia kelele wanazopigiwa wamiliki wa migahawa yenye mitandao kua wanapaswa kuhakiki mara kwa mara watu wanao pakua taarifa mtandaoni basi iwe ni taarifa tu na sio ngono! Lakini mara kadhaa tumesikia wanafunzi,wanavyuo na kada zote hawaachi kuingia mtandaoni kutafuta pilau na kuzitazama na mwishowe huondoka hapo na mhemko unaoweza kuwafanya wakabaka ama kupata mfadhaiko!
Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 12 amembaka msichana wa miaka 9 na hiyo ni matokeo ya kuangalia picha za ngono mtandaoni,amenusurika kufungwa jela jana na huku wakili wake akiionya jamii ya watoto na vijana walio katika vipindi vya mpito na hata walio komaa kutotazama picha hizo  maana hazina faida kwao zaidi ya kupandwa na pepo wa ngono anayeishia kuwatupa jela.
Kijana huyo kwa sasa ana miaka 14,anaeleza jinsi alivyo mbaka motto wa jirani yao lengo la kijana huyo ni kutaka kujiona amekua baada ya kuona kilichokua kinafanywa mtandaoni, nay eye anatoa ushuhuda kua hakua akifuatiliwa wakati akiwa mtandaoni na hiyo ikamrahisishia kufika alikofika na kutekeleza alichokidai kuji feel mkubwa!


                                                          dogo akiangali ngono mtandaoni.

Kufuatia kitendo hicho magazine ya Daily mail imeanzisha kampeni ya kufunga mambo ya ngono mitandaoni  Sean Templeton, ambaye ni wakili wa motto huyo anaeleza kua vijana wengi wanakua na kivuli cha mtazamo wa  ngono ni nini? Na shughuli nzima ikoje
Hakimu Lady Smith  aliamua kutoa maamuzi magumu na kusema kijana huyo asifungwe jela na badala yake achanganywe na watoto wenziwe na awe chini ya uangalizi
Mbaya zaidi binti aliyebakwa alimueleza mamake kitambo mbele kidogo kua anahisi akam kuna motto tumboni, alipotakiwa kufunguka alieleza kilichofanya na kijana huyo ,polisi waligungua kua binti huyo alikua mwathirika wa kufanyiwa udhalili huo katika bustani za nyumbani kwao kati ya December 1 na January mwaka 2011 ,kijana huyo alithubutu kumdhalilisha binti huyo akiwa katika chumba cha kijana huyo mbele ya rafiki yake.
Alipokua akihojiwa na polisi alionesha mtandao uliomhamasisha, na akahifadhi picha hizo na alijitetea kua ni mfadhaiko na kutaka kuwa mkubwa ndivyo vilivyo msukuma .baada ya maelezo hayo alitengwa mbali na jamii mile kadhaa mwanzoni mwa mwezi huu alionekana akitetemeka baada ya kusomewa mashtaka na kupatikana na kosa moja la ubakaji na udhalilishaji, atakua chini ya uangalizi hadi miaka 18 atakaposhtakiwa.



Lady Smith


Huo ni mfano huko mbele na ni tone la shtaka lililofika kwa pilato, yapo mengi, je Tanzania tunakilinda vipi kizazi chetu kinachopita katika vipindi vya mpito kisipelekwe na mihemko na kutaka kuwa wakubwa? Wangapi wamebakwa katika jamii zetu na wakaa kimya? Wangapi wamedhalilishwa na kuamua kukaa kimya kwa kuogopa endapo wakienda kushtaki watakua dhalili? Nini kifanyike ili kuvunja ukimya, na jamii inusurike na watu wanaokufa na vihoro kwa walichotendewa walipokua wadogo! Tuvunje ukimya, tafakari.

No comments:

Post a Comment