Friday, June 15, 2012

R.Kelly anadaiwa kodi ya dola 4.8 na Serikali ya Marekani


                                                                   Robert Kelly


 
Imearifiwa kwamba nguli R. Kelly  anadaiwa kiasi $4.8 milioni kwa kutolipa kodi ya mapato kwa miaka 7 sasa.
Mkali huyo wa wimbo wa The ‘I Believe I Can Fly’ aliacha kulipa kodi hiyo ya mapato tangu mwaka singer 2005, na hiyo ni kwa muujibu wa mashtaka aliyofunguliwa na Internal Revenue Service (IRS) kama TRA kwa hapa bongo.
Pamoja na ukubwa wa shtaka linalomkabili mshindi huyo wa tuzo za Grammy mara 2 mwenye umri wa miaka 45,  mwimbaji huyo ana jiamini na kusema kua suala hilo liko ndani ya uwezo wake hakuna tatizo!
Msemaji wake ameitonya  website  ya TMZ.com: Kwamba ‘R. Kelly yuko kwenye mchakato mzito wa kulishughulikia sauala kati yake na serikali na kila kitu kitakua sawa ,kinachoshangaza jamaa ameshauza mailioni ya rekodi zake lakini akaacha tu kulipa kodi ya mapato.

Kwa sasa anajipanga kuongoza tamasha la Reggae Sumfest  mwezi ujao huko Montego Bay, kuanzia  July 15 - 21.na ilikua aperfoam mwaka wa jana lakini aliahirisha kutokana na maumivu ya koo na baadae akafanyiwa upasuaji wa dharura wa koo


na huu ndo wimbo uliopata kupendwa na hauchuji hata leo! kwasababu ni sing along friday twende pamoja.

                 

No comments:

Post a Comment