Rais Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan anasema wakati
umefika raia wake kupanga uzazi. Kiongozi huyo amesema kuna watoto wengi sana
wanaozaliwa na ipo haja kuwepo na sheria ya kuwa na mpango wa uzazi.
Ameongeza
watu wasio jua kusoma wala kuandika wameendelea kuwapata watoto wengi ambao
wanashindwa kuwapa mahitaji muhimu ya maisha.Umoja wa Mataifa unakadiria idadi
ya Nigeria kuongezeka kutoka milioni 160 hadi milioni 400 ifikapo mwaka 2050.
Nigeria
inaongoza kwa idadi kubwa zaidi ya watu Afrika na juhudi za awali kuwashawishi
wazazi kuwapata watoto wachache ziligonga mwamba.Mwandishi wa BBC Will Ross
amesema ongezeko la watu linapunguza raslimali hali inayotishia kuwepo na
machafuko ya kushindania raslimali hususan ardhi.
Rais
Jonathan amesema ipo haja kuwepo na sheria ya kudhibiti idadi ya watoto wazazi
wanaopata katika siku za usoni.Amelitaka Baraza la Idadi ya watu kuanza
kampeini ya kushawishi jamii umuhimu wa mpango wa uzazi.
kina mama sokoni
Amesema
japo suala hili ni nzito kutokana na misimamo ya kidini na kimila, ipo haja
jamii kubadilisha mawazo kwamba watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment