Tuesday, June 12, 2012

Katibu Mkuu atoa 'Orodha ya Aibu' kuhusu watoto katika maeneo ya vita


Radhika Coomaraswamy Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa watoto katika maeneo ya vita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amewasilisha ripoti yake ya kila mwaka kuhusu watoto kwenye maeneo ya migogoro ya silaha kwa Baraza la Usalama, ambayo inatoa picha ya hali ya watoto katika maeneo ya vita na hatua zilizochukuliwa kuwalinda.
 Akiwasilisha ripoti hiyo, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa watoto katika maeneo ya vita, Radhika Coomaraswamy amesema kuwa mwaka 2011 ulikuwa na mseto wa picha ya matukio: wakati mizozo mipya ikizuka na kuwaathiri vibaya watoto kwenye nchi kama Syria na Libya, huku mingine ikimalizika kwenye maeneo mengine.
Miongoni mwa wahusika 52 ambao wapo kwenye orodha hiyo iitwayo 'Orodha ya Aibu', ni Sudan, Yemen na Syria. Kwa mara ya kwanza kabisa, Katibu Mkuu anaorodhesha maeneo ambako uvamizi umefanyika katika shule na hospitali, pamoja na kule wanakoingizwa watoto katika vita, kuuawa na kulemazwa, au kubakwa. Pia kwenye orodha hiyo yanapatikana makundi yenye silaha Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Iraq, pamoja na wanajeshi wa Syria wanaorusha makombora na kuchoma au kupora shule na hospitali.
wakati huo huo kuna taarifa zingine ya kua ,Mkuu wa ILO ataka hatua zichukuliwe dhidi ya ajira kwa watoto.

No comments:

Post a Comment