Wednesday, June 27, 2012

Askofu Afumwa Akila Bata, Picha zarushwa live Runingani






Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedict wa 16 ameikubali barua ya kujiuzulu ya Askofu wa Argentina na hiyo inafuatia baada ya picha ya Askofu huyo kuoneshwa hadharani hivi karibuni akiwa katika moja ya fukwe za mexico akiwa amekumbatiana kimapenzi na mwanamke aliyekua amevalia bikini

 

Askofu huyo aitwae FERNANDO BARGALLO, alipigwa picha hizo zikimuonesha akiwa amezama kibahaba na mwanamke aliyekua amevaa nguo za kuogelea zenye kuanika maungo yake yote yanayoonekana kumpagawisha Askofu FERNANDO

 
Askofu FERNANDO BARGALLO, alikua akihudumu katika jimbo la MERLO MORENO katika jiji la BUENOS AIRES na kashfa hiyo ilirushwa live na kituo cha television cha taifa hilo na kuonesha picha chafu za Askofu huyo akijivinjari wakati alipokua kwenye mapumziko katika fukwe tulivuuuuuuuu!

 
Kufuatia kashfa hiyo , tayari makao makuu ya kanisa katoliki huko VATICAN imemteua MONSIGNOR ALCIDES JORGE PEDRO CASARETTO, kuchukua nafasi ya askofu huyo aliyejiuzulu kwa hiari yake ili aendelee kula bata ,kwa uwazi na nafasi na mrembo wake.

No comments:

Post a Comment