Kila taifa lina utamaduni wake na vyakula vya asili vya
makabila yaliyomo katika taifa hilo.lakini vyakula vingine vinastaajabisha
kiasi cha ile methali ya Tanzania kupata mashiko zaidi, UKISTAAJABU YA MUSA!
UTAONA YA FIRAUNI!!
Nimeileta kwa sababu, huko china nyama maarufu iliwayo
sio ya ng’ombe,mbuzi na wengineo lah hasha bali mbwa,paka,mamba na wengineo
wamekua kitoweo maarufu kuliko kawaida, hivyo nitumie fursa hii
kuwatahadharisha watanzania wenzangu waendao China ambao pengine wana uchu wa
nyama wakiwa nyumbani, wajizuie kidogo katika nchi za watu wanaweza kulishwa
mifugo hiyo!
mbwa hao wameshanunuliwa tayari kwa biashara.!!!!
Kikundi cha Wanaharakati wa mjini Yulin, katika jimbo la Guangxi,
wamelipinga soko la biashara ya nyama ya
mbwa na kuwaomba watu wa eneo hilo kutokula nyama ya wanyama hao.
wanapelekwa buchani tayari kwa kuuawa,kuchinjwa ama kupelekwa katika soko la nyama la Guangxi.
Wachina walio wengi wana enjoy sana kula nyama ya mbwa, hasa kipindi cha majira
ya baridi na miji mingine huwapiga mbwa
hadi kifo ili kuruhusu damu ya mbwa itoke katika nyama.
Mpishi akikaangiza nyama ya mbwa , ona mwenye uchu unaweza kuingia mkenge! anaandaa mlo wa jioni.
tabasamu tele usoni dada huyu na familia yake wakipata mlo wa jioni , kitoweo nyama ya mbwa.utamaduni huu ni wa miaka mingi iliyopita.
sehemu ya machinjio,uchunaji na uandaaji wa nyama ya ng'ombe.
Wakati kukiwa na uhaba wa chakula, basi mbadala wa chakula
ni nyama ya mbwa kama chakula cha dharura maeneo mengi ya China utaratibu ama
zoezi ambalo limekubalika na Wachina walio wengi.
Mnamo mwezi April, zaidi ya mbwa 500 walikua wameandaliwa kwa kuuawa ,gari iliyokua
imewabeba kuwapeleka katika nyumba ya kuwachinjia ilipo zuiliwa na wanaharakati za wanyama.
Mbwa 505 waliokoka
katika hatari hiyo na hali za kuwadhuru na mbaya zaidi huwa hawanywi maji
wakati wa safari yenye urefu wa 1,000 kwa bara bara,ingawa mbwa 11 waliishiwa maji
mwilini na walikutwa na hali mbaya .
watu wakijisevia mgahawani ,kama uonavyo jibakuli liko kati jichotee tani yako.
mtaani anauzwa mbwa kama kawaida
unaweza kula nyama ya mbwa kwa tambi na mazaga zaga mengi tu! familia ikiendelea.
No comments:
Post a Comment