Friday, June 29, 2012

Kesi ya Rihanna Kupigwa Na Chris


                                       Rihanna

Polisi wawili wa jiji la Los Angeles hawatakabiliwa na makosa ya jinai kwa kuhusika kuachilia picha ya nyota wa pop Rihanna akiwa na madonda aliyoyapata kwa kupigwa na aliyekua mpenzi wake Chris Brown mahakama ya jiji hilo la Los Angeles imetoa tamko hilo
Na hii ni baada ya uchunguzi uliochukua miaka 3 ,wachunguzi wamedai kua hawana ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani maofisa hao.

Maofisa hao ni Blanca Lopez na Rebecca Reyes pamoja na kuepuka kuingiza hatiani, bado hawako salama, watatimuliwa kazi kwa kukosa nidhamu kazini.na kutakua na kikao cha kinidhamu mnamo mwezi August.

                                      Rebecca Reyes

                                        Blanka Lopez

                                            Chris na Rihanna

Brown, ambaye alikua ni mpenzi wa  Rihanna's  wakati huo alikamatwa kwa kumpiga mshindi huyo wa tuzo za Grammy winner mwezi Feb.tarehe  8,  mwaka 2009, na kumuachia majeraha na mvio wa damu.
Na hivyo kusababisha aahirishe kufanya show kwenye tuzo za Grammy mwaka huo kufuatia ajali hiyo.
Brown alikutwa na hatia ya kumshambulia Rihanna aliamuriwa kwa miaka mitano kua chini ya uangalizi na kutimiza miezi 6 ya huduma za jamii,ikiwemo usafi wa barabra na mengineyo
Reyes na Lopez walikua wanakaa chumba kimoja wakati huo walimpiga picha Rihanna na kuzitupia kwa watu wa Fox Television na TMZ mnamo mwezi February.

                                          Picha Za TMZ

Picha ambazo ziliwashtua mashabiki wa Rihanna na Brown na kuzusha mjadala mzito kabla hata hazijatua katika vyombo vingine vya habari. Na walilipwa mijihela ila walipofuatiliwa katika accounts zao bank hawakukutwa na kitu
 Katika kutaka kuwaonesha askari hao wathibitishe kua hawakuhusika kuachilia picha za Robyn F. (Rihanna) kwa  TMZ  kwa mabadilishano na pesa laikini pia wanakabiliwa na shutuma za kushadidia uhalifu kwa kusambaza picha hizo.
Wakili wa Rihanna aitwae Donald Etra jana alisema kua hajui kama mteja wake atahitaji kwenda mbele kisheria zaidi ama lah!


No comments:

Post a Comment