Monday, June 4, 2012

Zantel yaja na Huduma Mbili Mpya



Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel,imezindua huduma mbili mpya maalumu kwa wateja wake ambazo ni Epic Moto na Epic Bongo Star Search kwa lengo la kuwasaidia wateja wake kupata huduma za mawasiliano kwa bei nafuu.Akizindua huduma hiyo jijini Dar-es-Salaam mkurugenzi mtendaji wa huduma hizo Awaichi mawala amesema,wateja wake watafurahia huduma hizo kwa kupiga simu shilingi moja kwa sekunde kwenda mtandao wowote,kupiga bure Zantel kwenda Zantel usiku pamoja na kifurushi cha megabaiti 50 kila mwezi.

Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa biashara wa Zantel,Ahmed Mokhles ameiomba jamii na watanzania kwa ujumla hususan vijana kutumia huduma hizo sasa katika msimu huu wa Epic Bongo Star Search.

No comments:

Post a Comment