Marehemu Prof George Saitoti
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, ameelezea kuhuzunishwa kwa kifo cha Profesa George Saitoti, ambaye alikuwa waziri wa usalama nchini Kenya.
Katika taarifa yake, Mkurugenzi wa UNEP Achim Steiner, amesema wamepokea habari hizo za kifo kwa mshtuko na huzuni kubwa.
Bwana Saitoti alifariki dunia mwishoni mwa wiki kwenye ajali ya ndege, pamoja na waziri msaidiz katika wizara ya usalama wa ndani, Joshua Orwa Ojode na watu wengine walokuwa kwenye ndege hiyo.
No comments:
Post a Comment