Tuesday, June 5, 2012

Ugaidi unaendelea kuathiri maeneo yote duniani:Ban



Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon ,ameeleza kua Kuna haja ya haraka ya kukabiliana na ugaidi, kwani ugaidi unaendelea kuathiri maeneo yote duniani, na umeharibu maisha ya mamilioni ya watu na kufuta matumaini ya amani na maendeleo .
Akizungumza Jumapili kwenye mkutano wa pili wa bodi ya ushauri wa kituo cha Umoja wa Mataifa cha kupambana na ugaidi mjini Jeddah Saudia Ban amesema licha ya machungu na athari zote dunia inakabiliana na uhalifu huu.
Mkakati wa Umoja wa ataifa wa kupambana na ugaidi duniani uuliopitishwa bila kupingwa na wajumbe wote kwenye Baraza Kuu ni kiungo kikubwa cha juhudi za kimataifa kupambana na ugaidi. Ban amesema kimikakati dunia inahitaji kujaribu kuelewa na kupinga ugaidi, hii ikimaanisha kujenga utamaduuni wa kjadili sala hili, kuelimisha na kuchagiza mahusiano ya kijamii.

No comments:

Post a Comment