Saturday, June 30, 2012

Lauryn Hill Huenda akakabiliwa na Miaka Mitatu jela


                                                Lauryn Hill

Kama utakumbuka niliwahi kuandika humu bloguni kuhusiana na kesi inayomkabili mwanamuziki magiri,mzuri na mwenye ngozi mwanana Lauryn Hill kwa kutolipa kodi.
Hivyo basi, Kwenye Mahakama moja ya New Jersey , kesi ya Lauryn Hill iliendelea kusikilizwa  ambapo staa huyu wa muziki yuko kwenye hatari ya kwenda jela kwa miaka mitatu kutokana na kukwepa kulipa kodi ya dola za kimarekani milioni 1.8 kati ya 2005 and 2007, ambapo atatakiwa kuanza kutumikia kifungo chake November mwaka huu.
Kwa muujibu wa  AP Staa huyo amekutwa na hatia baada ya kukiri kwamba alishindwa kulipa kodi kwa sababu za kuikimu familia yake,  kitu ambacho ni kosa la kisheria
mmsanii huyo aliyetwaa tuzo za grammy mara 8,mwenye miaka 37 ,alikhukumiwa mwezi huu kwa kushindwa kulipa kodi ya Internal Revenue Service miaka kadhaa.Na alipotakiwa kukubali kosa ama kukataa, Hill alikubali kosa kwa kusema ndio sijalipa kodi kwa miaka hiyo yote.
Kwa muujibu wa wakili wa mwanamuziki huyo Nathan Hochman, Hill  amekubali kulipa kodi anayodaiwa  . Hill alikubali kua hajalipa kodi kwa mapato yake kama dola za kimarekani 818,000 alizopata mwaka  2005, dola 222,000 alizopata mwaka 2006 na dola  761,000 alizopata mwaka  2007.
Mbali na kukubali kulipa kodi anayodaiwa atapigwa fine ya dola 75,000 .Hill aliachiliwa kwa gharama ya dola 150,000  , na hukumu ya kifungo chake itasikilizwa November mwaka huu.

No comments:

Post a Comment