Wednesday, June 6, 2012
Shirika la ndege la Dana lapokonywa leseni
Mamlaka ya safari za ndege nchini Nigeria, imelipokonya leseni ya biashara ya shirika la ndege linalomiliki ndege la DANA iliyoanguka mjini Lagos siku ya Jumapili na kusababisha vifo vya watu 150.
Mamlaka hiyo ilisema kuwa shirika la ndege la Dana Air, halitaendesha safari zake za ndege tena hadi itakapochunguzwa kikamilifu.
Jamaa za waliofariki kwenye ndege hiyo wanajaribu kutambua miili za jamaa wao ambayo iko kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mjini Lagos.
Afisaa mmoja wa mamlaka hiyo, alisema kuwa rubani alikuwa ameelezea kuwa ndege ilikuwa na matatizo ya kiufundi kwenye injini zake mbili, kabla ya ndege hiyo kuanguka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment