Tuesday, October 16, 2012
TATHMINI YA UMOJA WA MATAIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO
Balozi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi, akizungumza siku ya Jumatatu,wakati wa Uzinduzi wa Tathmini ya Miaka Minne ya Shughuli za Maendeleo za Umoja wa Mataifa ( QCPR). Uzinduzi ambao umefanyika wakati wa Mkutano wa Baraza la Uchumi na Fedha ( ECOSOC)la Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa. Tanzania ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo. Katika mchango wake Balozi aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili hali halisi ya matatizo ya kiuchumi , kuongezeka kwa umaskini na upunguaji wa misaada ya kimaendeleo kwa nchi hasa zinazoendelea na nafasi ya Umoja wa Mataifa katika ufadhili na usimamiaji wa miradi ya mendeleo badala ya nchi wanachama kutumia muda mwingi kujitafutia uhalali na umaarufu. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson.
Friday, October 5, 2012
CHRIS BROWN ASIKIA KILIO CHA RIRI
Chris Brown ameonekana akiwa katika uwanja wa ndege wa Los Angeles ... na inadhaniwa amepungua kama 90 pounds. Hivi! Na hiyo inatanguliwa na tamko alilolitoa muda mfupi tu kua amemuacha girl friend wake Karrueche Tran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wake wa kirafiki na Rihanna
Baada ya tamko hilo Karreuche na ulimwengu wanaamini kwamba Chris Brown na RiRi walikua na mahusiano ya kisirisiri.
DUNIANI WAWILI WAWILI, NIMEAMINI! BONGO TUMETISHAJE?
Rick Ross wa
Bongo kumpokea airport Rick Ross wa Marekani, ama kweli duniani wa wili wa wili
Thursday, October 4, 2012
WATANZANIA SASA KUPATA BIMA KUPITIA M-PESA
·
Ni ushirikiano kati ya Vodacom na Heritage Tanzania
kuzindua bima ya Faraja, Bima ya mazishi na ajali.Wateja kununua na kulipia Bima kupitia M-Pesa.
·
·
Huduma ya bure kutolewa kwa wateja watakaolipia huduma
mara kumi kwa Mwezi.
Dar-es salaam, Octoba 3, 2012
… Huduma ya Vodacom ya M-Pesa
imezidi kupiga hatua baada ya kuwawezesha Watanzania kufanya malipo yao ya bima
kupitia huduma hiyo.
Hii inafuatia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na Heritage Tanzania
kuzindua Bima ya Faraja, ambayo ni Bima ya mazishi ambayo inamuwezesha mlengwa
kulipwa fedha taslim za mazishi kwa muhusika mwenye bima. Bidhaa mbalimbali
ziko katika mpango huo ili kukidhi mahitaji ya wateja na bajeti ya malipo ya
kila mwezi kuanzia shilingi 20000/= fadi 9800/= kwa Mwezi.
Mteja ana chaguo la kuongeza malipo kwa kuongeza huduma ya vifo
vinavyotokana na ajali kulingana na faida na sera zao. Ongezeko hili la ziada
litaongeza kiasi cha faida mara tatu kwa ongezeko dogo la malipo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema wateja wa Vodacom
wanaotumia M-Pesa, wataweza kujipatia bima ya bure kwa mwezi.
“Wateja wetu wote ambao watafanikiwa kutuma pesa walau mara 10 kwa Mwezi
watapata bima ya bure ya kiasi cha
Shilingi laki mbili kwa mwezi unaofuata,” amesema Meza.
Suala la kipekee katika huduma hii ni kwamba hakuna haja ya kujaza fomu ili
kujiunga na bima hii. Mteja atajiunga kwa njia rahisi kwa kupiga *150*00# na
kuchagua kipengele cha bima. Vodacom inahakikisha kuwa wateja wote wa M-pesa
wanaweza kupata huduma hii ili kuwa na amani ndani ya familia zao.
“Ni muhimu kuthibitisha kuwa taarifa
zako ni sahihi, na kuthibitisha kuwa unaelewa vigezo na masharti. Taarifa zako
zitatumwa moja kwa moja kwenda Heritage Tanzania,” alisema Meza na kuongeza
kuwa, “Unaweza kuchagua aina ya bima ambayo inakidhi mahitaji na bajeti yako,”
Bima hii ya Faraja
pia itawawezesha kila mmoja kubadili au kuongeza kiwango chake kwa ile yenye
faida zaidi kulingana na mahitaji yao na mabadiliko ya bajeti katika maisha
yao.
Kwa taarifa zaidi
kuhusiana na huduma mteja atapiga 0764 300001 bure au vipeperushi kutoka kwa
wakala wa M-Pesa nchini.
Mwisho
… ///
FIESTA DAR-ES-SALAAM HAH MAANDALIZI YANAENDELEA!!!
Nilipotembelea
viwanja vya Leaders Club hapa jijini Dar-Es-Salaam , kwenye harakati za kuangalia
vitu kwa jicho la tatu nilikuta mambo yanaendelea kama yalivyo pangwa, nikakuta
vitendea kazi viko eneo la tukio tayari kabisa kuusimika muonekano mpya lakini
burudani ileile! Hah!
Jukwaa
limeanza kupata muonekano huu, baada ya kuunga unga vyuma , likitayarishwa kwa
ajili ya mnyama! The big boss himself Rick
Ross kukwea October 6 mwaka huu! , tel your friend , tel your Friend
hah! Muonekano mpya burudani ni ile ile. Ticket utazipata hapa Clouds House,
Escape 2 , Robby One Fashions, Born to Shine Mwenge karibu na TRA na
kwingineko, huko utapata tiketi kwa tshs kwa 20,000/- na ukija mlangoni ni tshs
25,000/- kwa Serengeti Fiesta Bhaaaas! Usisite njoo na rafikiyo to parrrrtyy!!
Tuesday, October 2, 2012
BUSU HUONGEZA AFYA YA MWILI! NDIYO!
HIZI NI FACTS JUU YA BUSU NA NAMNA YA KUBUSU !
Kwa kawaida huwa tunatumia misuli miwili tu ya uso tunapotoa busu kwa rafiki ama mzazi, lakini linapokuja suala la kumbusu mpenzi ama mume basi huwa tunatumia misuli yote ya uso kumbusu umpendaye nah ii husaidia kuunguza calories nyingi zaidi wakati wa busu kwa mpenzi!
Monday, October 1, 2012
FIESTA 2012 MPANGO MZIMA - THE BOSS
Alipewa jina hili na wazazi wake William Leonard Roberts II tarehe yake ya kuzalizaliwa inatajwa kama January 28, 1976, lakini katika majukwaa ya muziki anafahamika kama known by Rick Ross mara zote akalipa swag jina hilo la kazi as RICK RO$$, akiwa anapeperusha bendera kama ni rapper wa Kimarekani. Ross alivumbua record label Maybach Music Group, huko akatoa album yake iitwayo Deeper Than Rap mnamo mwaka 2009 na album ni Teflon Don ya 2010. Mwanzoni mwa mwaka huu wa 2012, MTV ilimtambulisha Ross kama Hottest MC In The Game.
Subscribe to:
Posts (Atom)




