Tuesday, October 23, 2012

UAMSHO MAHAKANI WASOMEWA MASHTAKA

Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao.

Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.

Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi

RAIS KIKWETE KATIKA KILELE CHA MKUTANO MKUU WA UWT DODOMA



Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
             Mwenyekiti wa UWT mheshimiwa Sofia Simba akiongea jambo lililo chechemua meza.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)

VIFAA VYA KUFUNDISHIA VINAHITAJIKA

 Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa shule ya Buguruni Viziwi mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo airtel walitembelea shule ya msingi viziwi kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA, kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo bi Judith Kaneno akifuatiwa na Airtel Ambassador ajulikanae kwa jina la AY( Ambwene Yessaya) kulia ni Mwalimu mkuu bi. Winfrid Jeromia

 Mwalimu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi akiwapa ujumbe wanafunzi wa shule hiyo baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Airtel, kutoka kushoto ni mwamlimu mkuu wa shule hiyo bi Winfrid Jeremia, akifuatiwa na Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Airtel Ambassador Ambwene Yesaya (AY).  Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia

Monday, October 22, 2012

Mh. Lowassa katika uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya VOCOBA jijini Dar




Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.


Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.

   
                                       Burudani ya Ngoma za Asili.

WOMEN IN BALANCE YAPATA MWITIKIO NA YAFANA SANA!!!




Kiukweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, women in balance Kitchen party gala ilinoga mno! Mi nilikuwepo, watu walifurika na kupitiliza! Na hii ni ishara nzuri kwamba mkutano huo umekua na pnahitajika juhudi za dhati tena za makusudi kuiimarisha ili kuwakomboa wanawake na wanaume katika fikra mgando zinazoyumbisha ama hata kusambaratisha ndoa zao! 



Watu wakaanza kuingia! Huyo mwenye skirt ya orange na blaizer nyeusi ni Babra Hassan wa Power Breakfast  Clouds Fm


Ukaguzi ni muhimu popote pale, basi ilibidi subra ili ukaguliwe! Na mdada white ni Mrs Urio


                        Nyomi lilikua hivi! Na huu ni upande wa kushoto wa jukwaa! Walifurika babake

Friday, October 19, 2012

AT aka MFALME WA MDUARA Feat. DEPLAZIR LIVE ON STAGE @ THE CHAPLE LOUNGE LONDON 3 NOVEMBER 2012.




AT aka Mfalme Wa Mduara feat Deplazir Live on Stage @London The Chapel Lounge ig1 2af Sat 3rd November One Show Only..! Hosted By BongoDeejays |Chriss Luv Promotion| Jestina George Blog, So Get Your OutFit Ready Let Make it Happen Catch you there..! 

IT'S A BLACK & WHITE AFFAIR!!!
SO TELL YOUR FRIEND TO TELL A FRIEND

UNDP YAIPONGEZA TANZANIA KWA JITIHADA ZA MAENDELEO




 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akielezea jinsi shirika hilo linavyoshirikiana na serikali ya Tanzania katika kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kwenye kukuza uchumi.