Monday, May 28, 2012

Lady Gaga avunja Onesho lake Baada ya Kupokea Vitisho


Lady akiongoza makamuzi kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards



Mwanadada mbunifu wa maonesho ya jukwaani Lady Gaga ameahirisha tour yake ya kimuziki Asia baada ya kutakiwa kufanya hivyo na watu wa usalama wa Indoneshia baada ya tishio kutoka kwa viongozi wakuu wa kiislamu nchini humo.
Nyota huyo wa miondoko ya pop alikua akiipigia promo  album yake ya born this way ball ,ilimpasa kuahirisha show yake baada ya kuelezwa ukweli kua akitia mguu wake katika jiji la Jarkata basi ajue watashughulika naye.
Chama cha kutetea uislam The Islamic Defenders Front (FPI) kilitoa msimamo wao juu ya mavazi ya Lady Gaga kua yana shawishi ngono na uchezaji wake vinaweza  kuwatia majaribuni vijana wa Indoneshia na waislamu walio wengi katika taifa lao.na wakatamka wazi kua Gaga akijitia kichwa ngumu basi watamdhuru na wakamwita wakala wa shetani ambae huvalia sidiria tupu na chu** tu.
Pamoja na matangazo kibao kufanywa lakini management ya Gaga  wanatazama kitisho hicho kwa jicho la tatu na kuita kua ni lengo la kushusha moto wa tamasha la june 3 atakalofanya Gaga , ndipo mwanasheriaMinola Sebayang  ambaye ni promoter wa Big Daddy Promotion alipomtaka Gaga kuahirisha tour hiyo na kusema kua hawatawasamehe walowatisha .
Chama hicho cha FPI kimeendelea kueleza kua Indoneshia italindwa na kuepushwa na dhambi zitakazo sababishwa na shetani huyo,japokua chama hicho chenye mrengo wa kiislam kutoa vitisho hivyo! Raia wa nchi hiyo tiketi zipatazo 50,000 zilisha uzwa na ilitegemewa kua ndo tour kubwa kuliko zote kuwahi kufanywa Asia.
Management ya Gaga imeshangazwa na wana usalama wa Indoneshia walipowataarifu kua kutokana na sababu za kiusalama Tour ya Gaga katika nchi yao haitowezekana,serikali ya nchi hiyo ilishaonesha ushirikiano ,lakini tishio hilo ni kubwa kuliko mtu kukosa kibali cha kuingia katika nchi hiyo.
Saa chache kabla ya tangazo hilo kutolewa,mwanamuziki Lady Gagag mwenye follower milioni 25 katika account yake ya twitter alitupia kauli hii "There is nothing Holy about hatred."
Mwenyekiti wa chama hicho cha FPI ambaye anadai ana followers milioni 7 kwenye akaunti yake ya twitter wamefurashishwa na uamuzi wa Lady Gaga kutokwenda nchini kwao, awali FPI  wamesha shambulia  clubs na pubs kibao  na wamewataka mashabiki wa Lady kuacha kulalama na wajirekebishe na kama haitoshi waache kumwabudu shetwan.
FPI wanaendelea kufunguka kuwa wao kama wao walisha nunua tiketi kama 150 hivi ili kupata nafasi ya kua sehemu ya washiriki ili wapate nafasi nzuri zaidi ya kusimamisha show hiyo endapo ingelazimu kufanywa.
Kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali na pia mwenye dhamana ya mahusiano ya kidini  waziri Suryadharma Ali amefurahiwa na vuguvugu hilo la kumsimamisha Gaga kwa kufanikiwa kufanya hivyo na akasherehekea kufanikiwa huko na kusema kuahirishwa kwa tour hiyo ni kwa manufaa ya nchi yao  na kueleza kua Indoneshia burudani haikataliwi mradi iwe ya kistaarabu  na si vinginevyo  no!
Pamoja na FPI kumtia mkwara Lady Gaga, kuna waliotangulia kufanya show nchini humo kama Beyonce na Pussycat Dolls wao walisoma alama za nyakati na kuvaa vyema ili tu wapaafom na walifanikiwa.
Pamoja na hayo yote Maelfu ya followers wa Gaga walimtumia tweet kibao wakimtaka Gaga asihofu chochote bali aendelee na mipango yake kama kawaida, kijana mwenye umri wa miaka 17 Agus Murdadi amesubiri kwa  miezi kadhaa kumuona Lady Gaga ,na akaeleza hisia zake kua ameshtushwa sana na taarifa kua Lady Gaga hata kwenda tena nchini mwao kwa mtazamo wake Lady ni mbunifu na sio mhamasishaji ngono.na kuahidi kumtumia tweet Lady kua asihofu aende tu nchini mwao na kusema polisi wanaweza kuwazui FPI wasifanye chotechote nay eye kwa nafsi yake anawachukia FPI.
Lady Gagag ana show zipatazo kama 3 hivi , huko Singapore wiki hii  kabla hajakwea pipa kuelekea New Zealand na Australia na baadae Ulaya kumalizia tour yake.


                                                           Lady Gaga

Mtumishi wa Papa Benedict akamatwa


Basillika hiyo.



kwenye duara ni mtuhumiwa Paolo Gabriele akiwa na Bosi wake Papa Benedict wa xvi



Jana ilikua ni siku ya kumuabudu Mungu kwetu sisi wakristu, wengi walijitokeza katika nyumba za ibada, kwa wakatoliki kama mimi mkuu wetu ni Papa Benedict wa xvi, makao yake makuu yako Roma nchini Italia.kuna jambo huko mjengoni ambapo ,Polisi wa Vatikani wamemshtaki rasmi mtumishi wa Papa Benedict, katika kesi inayohusu wizi wa nyaraka za siri.
Paolo Gabriele - ambaye alikua akitumika kwenye fleti ya papa - amezuwiliwa Vatikani, na ameruhusiwa kuonana na mawakili wawili.
Wakuu wanachunguza vipi, katika miezi ya karibuni, magazeti ya Utaliana yalipata nyaraka ambazo zinaeleza mashindano kati ya wakuu wa kanisa - kisa ambacho kimeanza kuitwa 'Vatileaks'.
Inaarifiwa kuwa Papa Benedict ameshangazwa na kusikitishwa kuwa mtumishi wake mmoja amekamatwa.




Mkuu wa Benki ya Vatikani alitolewa kazini Alhamisi, kutokana na kashfa hiyo.

Friday, May 25, 2012

Picha za Siku ya Leo


Mungu kweli anaumba! kindege kinatabasamu hadi kimefumba macho, halafu Mungu akampamba kwa hiyo rangi juu ya macho yake sijui niseme nyusi? kazurije? wow asante Mungu kwa uumbaji.



wako katika mazoezi ya yoga, Mungu ni waajabu sana wanyama wakifundishwa kwa Lugha zetu wanaelewa na kufuata maelekezo yote uwapayo.mbwa ni rafiki muaminifu na mlinzi mzuri sana mi huwa napenda aina ya mbwa kama wale wa feed Force.






Picha ya Leo


hii ni picha ya leo nimependa alivyopambwa! zaidi sana kicheko chake ndege huyu!

Will Smith Asafishwa


Willy Smith

juzi kazi willy Smith alibusiwa na tv Presenter na yeye Willy akamtumbuiza kwa kofi! naamini unakumbuka au siyo? so  jamaa ameomba radhi na kuahidi kutorudia kumbusu na badala ya akikutana naye atamsalimia kwa mkono tu




Will Smith akifafanua namna tukio lilivyotokea na alikua akihojiwa na Mr Letterman



 na hapo chini jamaa naye anafunguka juu ya tukio hilo.


JOHN MNYIKA AIBUKA KIDEDEA MAHAKAMA KUU JANA



Mbunge wa jimbo la Ubungo CHADEMA Mh. John Mnyika akiwa amebebewa na wanachama wa chama hicho mara baada ya mahakama Kuu ya Tanzania  kumtangaza mshindi katika  kesi ya uchaguzi iliyokuwa ikimkabili  kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Ubungo iliyofunguliwa na mpinzani wake Hawa Ng'humbi wa chama cha CCM.


John Mnyika akionyesha ishara ya ushindi akiwa na wapambe wake pepembeni wakielekea Ubungo kwa ajili ya mkutano wa hadhara



John Mnyika akiutubia wafuasi wa chama chake katika jimbo lake la Ubungo mara baada ya kuwasili



Jeshi la polisi likihakikisha ulinzi unaimarika katika mahakama hiyo leo.

Thursday, May 24, 2012

Tuzo Za BET zaja








Host ndo huyo naamini mwamfahamu kupitia thamthilia ya  Isidingo The Need Samuel L. Jackson


Tuzo za BET zaja na zitakua mwezi July 1, jijini Los Angeles nchini Marekani.wafuatao watachuana kuwania tuzo kama mtiririko huo hapo chini unavyo ainisha.

Best Female R&B Artist:
Marsha Ambrosius
Beyoncé
Mary J. Blige
Melanie Fiona
Rihanna
Best Male R&B Artist:Chris Brown
Bruno Mars
Miguel
Trey Songz
Usher
Best Group:Bad Meets Evil
Diddy-Dirty Money
Maybach Music Group
Mindless Behavior
The Throne (Jay-Z & Kanye West)
Best Male Hip-Hop Artist:Big Sean
Drake
J. Cole
Lil Wayne
Rick Ross
Young Jeezy
Best Female Hip-Hop Artist:
Diamond
Nicki Minaj
Brianna Perry
Trina
Best International Act: UK:
Estelle
Labrinth
Emeli Sandé
Sway
Wretch 32
Best New Artist:A$AP Rocky
Big Sean
Diggy
Future
Meek Mill
Video of the Year:Beyoncé - 'Countdown'
Beyoncé - 'Love On Top'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) - 'N***as in Paris'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) featuring Otis Redding - 'Otis'?- Usher - 'Climax'
Viewers' Choice Award:
Beyoncé - 'Love on Top'
Chris Brown - 'Turn Up the Music'
Drake featuring Lil Wayne & Tyga - 'The Motto'
Mindless Behavior -  'Hello'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) featuring Otis Redding - 'Otis'
Wale featuring Miguel - 'Lotus Flower Bomb'
Best International Act: Africa
Camp Mulla (Kenya)
Ice Prince (Nigeria)
Lira (South Africa)
Mokobe (Mali)
Sarkodie (Ghana)
Wizkid (Nigeria)
Best Collaboration:
Beyoncé featuring J. Cole - 'Party'
Big Sean featuring Kanye West & Roscoe Dash - 'Marvin & Chardonnay'
DJ Khaled featuring Drake - Rick Ross & Lil Wayne - 'I'm On One'
Drake featuring Lil Wayne & Tyga - 'The Motto'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) featuring Otis Redding - 'Otis'
Wale featuring Miguel - 'Lotus Flower Bomb'



Beyonce

bibi huyo hapo juu ameingia katika category 6 tofauti tofauti



Kanye West

yeye amekua nomineted mara 7



Chris Brown

anawania tuzo tatu ikiwemo ya Best Male RnB Artist  na ataburudisha katika sherehe hiyo ya utolewaji wa tuzo za BET


mabibi hapo juu wenye vibweka karibu sawa wanawania tuzo moja category tofauti



                                  Big Sean maetwaa tuzo 2 ikiwemo ya Best New Artist

tusubiri kuona  watazikwaa hizo nomination?