Thursday, September 6, 2012

Hayati Kadinal LAURIAN Rugambwa Kuzikwa upya!



                      KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA  1912----1997

Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  anatarajiwa kuwaongoza wakaazi wa mkoa wa KAGERA katika kumbukumbu ya kumuenzi aliyekua Askofu mkuu wa Kwanza wa kanisa Katoliki Tanzania Mwadhama KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA inayotarajiwa kufanyika oktoba sita mwaka huu mkoani humo.

Hayati Rugambwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete


                 Askofu mkuu msaidizi jimbo la Bukoba METHODIUS KILAINI

Akizungumza jijini Dar-Es –Salaam, Askofu mkuu msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Bukoba, METHODIUS KILAINI amesema kwamba katika hafla hiyo shughuli mbalimbali zinatarajiwa ikiwemo ile ya kuhamisha mabaki ya mwili wa Hayati KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA na kuhifadhiwa katika sehemu maalum kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

            KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA kulala upya humu


Hayati KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA , alizaliwa julai 22 mwaka 1912 na kufariki dunia Desemba 8 mwaka 1997 ambapo Rugambwa anakumbukwa kama cardinal wa kwanza Mwafrika na Askofu mkuu wa kwanza wa kanisa katoliki hapa nchini Tanzania.
July 12 mwaka huu alitimiza miaka 100 na october 6 mwaka huu atazikwa upya na hii ni kumbukumbu kuu si kwa Bukoba tu bali Tanzania na nchi jirani so kufanikisha hayo yote mawili kufanikiwa kifedha Askofu msaidizi ana ombi! Msije sema ni maneno yangu soma mwenyewe! To assist with financial costs, logistical planning, material, volunteer, email: Rt. Rev. Bishop Method Kilaini: mkilaini@gmail.com & Fr. Adeodatus Rwehumbiza: arweyhufr@yahoo.it


 natamani ningekuwepo! mwadhama hayati Kardinal Rugambwa alinipa komunio ya kwanza, nikacheza naye mziki na kula nikala naye, nakumbuka alivyoshika mikono yangu na kucheza nami, mi nlikua mfupi ye mrefuuu! mungu akulaze mahala pema peponi baba RUGAMWA! NAKUKUMBUKA, NA BADO NAKUPENDA BABA .

Michelle Obama Amnadi Mumewe




                                                          Michelle Obama
Mkewe Rais wa Marekani, Barack Obama, Michelle, amehutubia kongamano la chama tawala cha Democratic ambapo alitetea haki ya mumewe kupewa nafasi kutawala taifa hilo kwa muhula wa pili.
Akiongea Kaskazini mwa Jimbo la Carolina, alimtaja mumewe kama mtu anayeelewa matatizo yanayowakumba wamarekani.


                     Familia ikimshudia mama akiingia mkutanoni


                                      Mama akiingia mkutanoni


Salaam! mi utege na fitness yake tu! ingawa najua kui zingatia si mchezo, mazoezi!

Michelle Alitetea hatua ya mumewe ya kuanzisha mpango maalumu wa bima ya afya ulioleta utata mwingi sana hasa miongoni mwa wanachama wa chama cha upinzani cha Republican walioupinga.
Alisema kuwa mumewe alinuia kutoa nafasi sawa ya matibabu kwa wote. Hata hivyo alikiri kuwa mageuzi aliyoahidi mumewe miaka minne iliyopita yalikuwa magumu kuyatekeleza lakini akasisitiza kuwa yatafaulu baadaye.
Rais Obama atahutubia kongamano hilo baadaye juma hili, ambapo atakubali rasmi kuwa mgombea wa Urais wa chama cha Democratic.

Wednesday, September 5, 2012

Miti Yenye hasira Inayokula Alama na Kingo za Hadhari!!!!




Mungu anaumba kiukweli! Na uumbaji wake haudanyi, na leo naomba nikuoneshe uumbaji wa Mungu ambao hauna subra katika vilivyoundwa na wana adam pindi wanapoingilia, ama kuweka mbele,karibu na miti hiyo yenye hasira , kwani hakuna pengine pa kuweka mpaka kwenye miti? Kuizunguushia vitu inahusu nini? Na yenyewe inataka kujiachia!
Miti haina midomo, hutoa sauti na harufu nzuri za manukato yake ya  asili pindi upepo unapovuma ama kupuliza taratibu!
Miti imekua ikila alama za barabarani! Mawe ya makaburi, vibao vya chuma, huvimeza taratibu! Hadi vyote viishie ndani ya jimti hili! Leo wacha nikuoneshe nguvu na uweza wa Mungu iliyomo ndani ya miti! Pengine Mungu anasema nasi kupitia miti hiyo! Sijui najaribu kufikiri kwa njia ya picha!

Tuesday, September 4, 2012

Kucheka ni Afya, Naomba nikuongezee Afya!



hii nimeipata katika You tube !

Kulala kwenye basi ama train ni  numerrr, angalia video clip hiyo hapo chini ucheke kidogo! Ingawa mdada alikua anaona soo si kidogo!
Video hii imesababisha kila aliyeiona acheke mno! Lakini mke wa mshkaji hapo hakuelewa kama ulikua ni usingizi wa kawaida bali ameng’ang’a kua anataka kuibiwa ! na mbona mume haku react? Alitabasamu kwa raha tu! Ina maana kafurahia kilichotokea na alikua tayari zaidi au?

Rakesh Nair ndo jamaa alolaliwa anasema mkewe amemdindia kua wanajuana na huyo demu alo mlalia! Japo alijitetea mno kwamba wamekutana kwenye train hiyo! Aaaah wapi haeleweki, na mkewe anadhani kua inawezekana kua huyo demu ni mfanyakazi mwenziwe na hana raha maana anashutumiwa kwa kumuibia tundi lake! Lol mpaka anaoneshwa kwenye video? Imezidi
Nair and Paula Jovel ndo jina la huyo mdada alokua amekaa jirani na Rakesh walikua kwenye train ya chini jijini London njia maarufu iitwayo Jubilee line. Nair,kilichomfanya asinzie pengine ni  hiki  yeye ni chef mkuu katika London's Cinnamon Club, alikua akirejea home mida ya usiku mwingi baada ya kazi nyingi za mchana kutwa  na alikua akisinzia sinzia  na tumeweza kuona hii video baada ya rafiki wa mdada huyo kutumia cm yake kuchukua video namna rafikiye anavyo sinzia bila kujua nini kitatokea mbele , lakini si ajabu watu wa eneo analofanyia kazi Nair wengi wao hurejea nyumbani wakiwa hoi bin taabani.

Aliyejiita Masiha Aaga dunia


                                                        Sun Myung

Mwanzilishi wa kanisa lenye utata la Muungano wa kiroho na lenye mamilioni ya wafuasi duniani, Sun Myung Moon, ambaye aliwahi kujitangaza kuwa masiha amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.


                         Alichokianzisha! ndoa za halaiki


              Sung na Mkewe wakiwa na maharusi kikanisa zaidi


Baada ya kufunga ndoa, unapaswa  kuonesha furaha ya ndoa!  

Moon ambaye ameacha himaya kubwa ya kibiashara na kumbukumbu ya harusi za halaiki alipatwa na ugonjwa na nimonia na kupelekwa hospitalini mjini Seoul katikati ya mwezi uliyopita, kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya kijijini baada ya familia yake kuona kuwa hana dalili za kupona.

                                      Sung Myung na mkewe

Mwili wake ulilazwa katika jengo kubwa linalofanana na ikulu ya Marekani, na maafisa wa kanisa lake wamesema msiba utafanyika Septemba 15 na baadaye kuzikwa huko.


     waumini wakitoa heshima mbele ya picha ya kiongozi wao wa kidini

Sun Myung Moon Jina lake la kuzaliwa ni Mun Yong-myeong mnamo   25 February 1920 –  na kufariki 3 September 2012
Kanisa hilo inadaiwa lina waumini milioni 5 hadi saba duniani kote  na kanisa lake inadaiwa lina utajiri wa mabilioni ya dola yasiyoelezeka.

Monday, September 3, 2012

Meles Zenawi azikwa jana


Jana ndo mwana Africa Meles Zenawi alipopumzishwa katika nyumba yake ya milele, huu ni mfululizo katika picha.


Mwili wa Meles Zenawi ukipelekwa kwenye sehemu maalum ya kumuagaSifa na salamu zilitolewa juu ya waziri mkuu Meles Zenawi wa Ethiopia aliyeongoza kwa miaka mingi, ambaye amezikwa katika mji mkuu, Addis Ababa.

                                            Namna alivyobebwa


                               Jeneza la Meles Zenawi


          mwili  wa Meles Zenawi ukiwa katika sehemu maalum



            Itifaki ya kijeshi ilizingatiwa kwa heshima yake


                                 Kitamaduni zaidi!
Viongozi wa Afrika na kwengineko walionesha  heshima zao pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye alisema Bwana Meles alitumia upeo wake mkubwa kuendeleza Afrika

R.I.P Daudi Mwangosi


                                                Marehemu Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.

Mroki ni mwandishi wa habari na mmiliki wa mrokim.blogspot.com ameripoti kwamba mwandishi wa habari na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi amefariki dunia kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa baada ya kutokea vurugu kati ya polisi na wafuasi wa chama cha Chadema.
Mwangosi ambae ni mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel ten, amefariki papo hapo ambapo vurugu zilitokea katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa september 2/ 2012  saa kumi jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa kwa risasi .
Kabla ya kifo chake, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kwake  kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo alitaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kipigo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo ambapo mwandishi huyo pamoja na askari mmoja wakaanguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti ya askari huyo ikisema afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe na mabomu, zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa akiwemo mwanahabari mmoja Godfrey Mushi.