Thursday, August 23, 2012

Viatu Vyenye Kisigino zaidi ya Inchi 5 Ni hatari Ki afya

Viatu vyenye visigino virefu vinaweza kuwasababishia akina dada matatizo ya uzazi imebainika.

Dax Moy ambaye ni mtaalamu wa kuwafundisha walimbwende namna ya kupozi, anadai kwamba viatu hivyo hasa vile vinavyofikia inchi tano na zaidi, vinamlazimisha msichana kukaa katika pozi zisizo za kawaida ambazo husababisha matatizo ya uzazi pindi atakapo hitaji kua nao.

Licha ya akina dada wengi kutambua matatizo ya viatu virefu ya mgongo, enka na miguu, wengi wao hawajui kwamba viatu hivyo vinaleta madhara kwenye viungo vya ndani ya mwili hasa via vya uzazi.
Moja ya matatizo makubwa ni kwamba jinsi viatu vinavyozidi kuwa virefu, vinasababisha sehemu ya chini ya tumbo kuegemea mbele, ambayo huleta maumivu ya mgongo .

Sehemu ya chini ya tumbo ni kama chombo cha kuhifadhia viungo vya ndani ya mwili, kila kitu kinatengewa nafasi ya kufanyia kazi yake.

Sehemu hii ikibinuka kwa mbele, viungo vya ndani vinabaki vimepandiana na kukuacha ukijisikia kama una msongamano au mvutano kwenye maeneo hayo.
Msichana unapojisikia uzito kwenye sehemu za chini ya tumbo, mara nyingi ni kwa sababu viungo vya ndani ya mwili vinaegemea upande wa mbele ya tumbo.

 Na kwasababu hiyo basi! Hii inaweza kupunguza ufanisi ndani ya tumbo na kuleta matatizo ya hedhi ambayo hatimaye husababishia wasichana kushindwa kushika mimba  .

Mi nilishindwa zamani kuning’inia , na siweki hapa kuwavunja moyo! Lah hasha!  bali hii ni kwa taarifa yako tu! Enjoy your heels! Zitakazo kupa miondoko yenye kuvutia!  Naomba nikutakie asubuhi njema.

Wednesday, August 22, 2012

Chui akutana na Rafikiye wa Zamani Baada ya Miaka 13


                                                                              old friend eh!

Bwana  Alberto Lena ameungana tena na rafikiye chui mwenye jina ambalo siwezi kuliweka hapa kutokana na mila na desturi zetu kua ni tusi ama kiungo cha uzazi cha jinsi  ya ------- , amabye alikua  Shamwari Game Reserve huko Eastern Cape. Lena alimuokoa chui huyo kutoka kwa wawindaji haramu huko Ivory Coast  miaka 13  iliyopita.




Kawaida ni kama sheria! Unapokwenda kumtembelea mtu shurti ubebe zawadi! Jamaa alibeba zawadi kwa ajili ya rafikiye! akampa




bila shaka ni tamuuuuuu! au siyo? lakini je unamkumbuka mshkaji wako?mtazame tena basi!




baada ya kula akamtazamaaaaa! je unadhani anamkumbuka? sidhani




aaaagh vipi tena? urafiki umeisha mara? mbona zawadi ulikula?

kiukweli napenda sana wanyama! lakini urafiki na mnyama kama Simba,Chui, Tembo na wengineo mh hapana! wazuri kuwatazama kwa mbali na kutukuza uumbaji ila kwa karibu? labda awe kafa! sorry. kiukweli anaweza kukubadilikia anya time hapo tu mi ndo imani hua inantoka! HAWAFUGIKI!

Tuesday, August 21, 2012

Rihhanna a.k.a Robyn Fenty amuenzi mamake Mzazi (MONICA)


                                                                    Mama na mwana

Rihhana ni mwenye kukumbuka fadhila na kushare kile alichonacho na wapendwa wake, hivi karibuni alimpa mama yake mzazi Monica Braithwaite kile alichoona kinamfaa, na hii ilikua ni katika mahojiano na Oprah Winfrey ,zawadi hiyo ni nyumba ya haja yenye vyumba vitano mpya kabisa kwa heshima ya mama yake , nyumba ambayo iko eneo alikokulia  ,Barbados.



                      Hapa Rihanna anamuandaa mamake kupokea habari njema!



    Huwezi amini mansion hii ni yangu? you! Rihanna? me? oh myGod! mama alizuia pumzi zake



                     Mpyaaaaaaaaaaa, kwa mbele na kwa pembeni full mijiua





                         Kuzaa kuzuri jamani, kwa nyuma, mama kapewa sehemu ya kujiachia







                           Kiukweli Rihanna ali stahili hugg,! oh Mama! mama alichanganyikiwa kwa zawadi njema na kumtazama tu mwanawe! na alimwambia alitaka kumpa zawadi hiyo muda mrefu tu!



         Mama bi Monica akafanya ukaguzi wa nyumba yake mpya, mbele  ni aunt yake Rihanna!



                                Nyumba yao ya zamani Rihanna huko Barbados




                   Rihanna akimuonesha Oprah Maisha alikoanzia, ameishi hapo kwa miaka 11



             Baada ya hapo alimwagika machozi! why? ungana nami hapo chini!



Machozi hayo ni baada ya kurejelea yale yalotokea mnamo mwaka 2009, Rihanna alilielezea tukio hilo kua  lilikua la  kufadhaisha na la kinyanyasaji mno ambalo lilisababisha ampoteze rafikiye kipenzi
Na kueleza kua tangu katazo la kumtaka Chris asimkaribie Rihanna liondolewe mnamo February 2011  , basi wamekua wakijishughulisha juu ya suala la urafiki wao na wamekua karibu  na wanaonana sana tu kama mwezi ulopita walikua  St Tropez.na hawawezi kuubadili ukweli kua wao ni marafiki wa karibu ingawa ni ngumu kujiachia kwa  mpenzi wake wa zamani kwasababu hisia zake bado zinakinzana. Na mbaya zaidi bado anampenda. Na mtu asipozijua hisia zake basi anaweza kufanya makosa mengi mno!
Rihanna amainisha kua kuonana kwao si kimahaba kwani Chris tayari ana mpenziwe ambaye ni model Karrueche Tran, na yeye anabaki kua single na kumbukumbu za mahaba yao bado zinajirudia kichwani mwake kila uchao na anadhani Chris Brown  ndiye wake wa maisha na yeye ndiye aliyeanza naye.


Lakini katika wakati huu sasa! Rihanna anaonesha kweli amekomaa kwani anasema wakati ajali ilipotokea ya kupigwa na mpenzi wake, walikua bado wadogo walipoangukia mapenzini, wakaenda nayo mbio,na kujisahau wao wenyewe.
Na il kua na amani na kuvunja unyanyasaji ameamua kumsamehe baba yake  na kutengeneza upya uhusiano wao na baba huyo, Ronald Fenty.kwani mwanzo alikua na hasira naye , kutokana na mambo kadhaa yaliyotukia utotoni mwake na hakuweza  kutofautisha mume na baba! Na akatanabahisha hasira zake zatokana na unyanyasaji wa baba kwa mamake bi Monica.
Wazazi wa Rihanna walitengana miaka miwili kabla Rihanna ahajaondoka Barbados wakati huo Riri alikua na miaka  16. Rihana ameeleza kua tabia ya babake iliitenga familia yao. Japokua hakutaja makosa halisi! Na hii inathibitisha msamaha halisi kwa babake, na kwamba amejifunza kutoka kwa Chris Brown, na kwamba sasa maisha yaendelee baada ya miaka 3 ya kugubikwa na scandal ya kupigwa na mpenziwe wa zamani.
Naye anasema nami namnukuu 'I have to move on,' na . 'I have forgiven him. It took me a long time. I was angry for a long time.' Wow nimemsamehe,ingawa imenichukua muda mrefu! Maisha inabidi yaendelee! Nampenda sana! Kikubwa  ninachofurahia ni kwamba Chris ana amani kwa sasa, najali, ina maana kwangu kwamba ana amani tena.
Na ametoa wito kwa watu wanaomshangaa kumsamehe alompiga! Anasema hawezi kuzuia hisia zao, ilikua kitu mbaya wao kua na hasira ilikua sawa kwa kilichotokea, lakini nimemsamehe!

Sunday, August 19, 2012

Rihanna Akiri Bado Anampenda Chriss Brown





Mwanama mwenye historia nzuri katika medani ya habari na mahojiano mkubwa Oprah, hivi karibuni amefanikiwa kumtia katika kumi na nane zake  mrembo  Rihanna katika show yake   OWN network ,show  ya Oprah ambayo inaingia katika ukurasa mwingine sasa na kuwashika watazamaji na washabiki wa bi mkubwa huyo mahiri katika fani ya utangazaji na mahojiano
Tumemshuhudia binti wa miaka 24 akishusha mvua ya machozi wakati alipokua akimzungumzia  Chris Brown na mwisho wa mapenzi yao , lakini kwa sasa RIRI anaona kama historia tu , na mwimbaji huyo anakubali kua mahusiano yao baada  ya miaka 3 bado ana mhitaji kwani ana mmiss.

Kwa muujibu wa mahojiano hayo ya hivi karibuni this latest, Rihanna hahuzunishwi tu na mwisho wa mapenzi yao! Lakini anamkumbuka  Breezy kila iitwapo leo .
Na Rihanna anafunguka kile kinachomfanya amkumbuke kwa mengi , moja ni zile kumbukumbu nzuri walizokua nazo, mambo yenyewe si makubwa sana! Ni kama vile vyumba vya hotel,maeneo waliyotembelea,chochote kizuri,muziki walosikiza pamoja, nyimbo, na ana mkosa kwa nyakati hizo!
                                                       Breezy

Na Oprah akamchombezea Chriss   “She talks a lot, a lot, a lot about you know who, Mr. Chris Brown.”
Lakini pamoja na hayo, Riri hayuko na Breezy, RiRi aeleza anamtaka mwanamume wa aina gani ajaye :
 Hapa namnukulu    "I know what I want… RIRI anajua anachokitaka, kama itatokea tena anamtaka mwanamume anayempenda,atakaye nijali,atakayenithamini lakini anapaswa kuijua thamani yangu ili kunithamini  kwasababu RIRI mwenyewe anaijua thamani yake hivyo anataka kuheshimiwa . kama hiyo haitoshi anataka muda wa kujiachia mpaka baasi , anataka mtu atakayemfanya acheke muda wote, anapenda kucheka kuliko kitu chochote kwasababu ana kila kitu hivyo alivyovitaja anavihitaji zaidi na anachotaka kwasasa ni mshkaji, ama mwenza wa kufurahi naye
Pamoja na yote yalotokea  Rihanna na  Chris walikua na uhusiano wa muda mrefu wenye mahaba ya dhati , haya twasubiri nini Rihanna ataelezea juu ya mshkaji wake huyo wa zamani maan inaonekana yuko kichwani mwake na sasa anamuongelea.



Friday, August 17, 2012

Koffi Amdunda Produser wake?!


                        KOFFI OLOMIDE

Mwanamuziki mashuhuri barani Afrika, KOFFI OLOMIDE ameshitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki makofi na kuumizi mdomoni.
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani siku ya jumatano kutokana na kuhusishwa na vurugu zilizotokea katika hoteli moja mjini Kinshasa na wakati wa vurugu hiyo inasemekana Koffi aliharibu baadhi ya mali za hoteli hiyo ukiwemo mlango wa hoteli hiyo na mali kadhaa za Lubaki ziliharibiwa.



Watu wengi walijitokeza katika Mahakama hiyo ya Kinishasa kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo imeharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.Wakati wa kesi hiyo KOFFI OLOMIDE aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake wa album ya Adakadabra  Bwana  DIEGO LUBAKI, ni kuhusu pesa dola $3,680


                                                     Diego Lubaki


Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Mmoja wa mawakili wa waliokuwa wakimtetea Mwanamuziki huyo LWEMBA MUYABO amesema walikuwa wanaamini kuwa mteja wao ataachiwa kwasababu promota alikubali kuondoa kesi hiyo.

Mashuhuda watatu wote waajiriwa wa  hoteli hiyo ya Venus,walitoa ushahidi wao kwa alichokifanya Koffi kwa alichomfanyia Lubaki

Wawili kati ya hao walisema kua walimwona kiongozi wa bendi hiyo ya orchestra Latin Quarter akimpiga Diego Lubaki, wakati wakigombea suitcase ambayo inadaiwa kua ni mali ya Lubaki .
Shahidi watatu ambaye ni menejwa hoteli hiyo ambaye ni mwana mama alisema kua alimwona Koffi akiingia katika chumba ambacho  Diego Lubaki alikua akikaa bila watu wa mapokezi kutaarifiwa  
Wawili wa mwanzo walisema kua walimwona Koffi akiwa amebeba   elevator kuelekea kwenye chumba cha Diego.
Hata hivyo kutokana na mchanganyo huo wa mambo upande wa utetezi ulijinasibu kua hakuna ushahidi wa dhiri na kudai kua mteja wao hana hatia.

Chumba cha Mahakama kilifurika wasanii kibao,waandishi habari ambao Koffi huko nyuma pia aliwahi kumpiga walau mmoja na washabiki wa Koffii pia walikuwepo , na wawili kati yao walitiwa ndani kwa makelele ya kumtetea Koffii kua hana hatia.

Antoine Akgepa, Alias Koffi Olomide mwenye mchanganyo wa congo-Sierra Leoneaalizaliwa  August 13, 1956 huko  Zaire ya zamani leo hii ni jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Koffi ndoto zake ilikua aje kua mcheza mpira mahiri duniani lakini alipokua motto alianza kuvutiwa na muziki taratibu! Akiwa mapumzikoni mnamo mwaka 1978 mjini  Kinshasa alirejea likizo kutoka Ufaransa alikokua akisoma na akarekodi wimbo wake wa kwanza mnamo mwaka 1983 ndio mwaka wa safari yake ya kimuziki ilipoanza rasmi kwa album ya Ngounda.
Baada ya miaka 3 akaunda kundi maarufu hii leo la Latin Quarter ambalo kiongozi alikua yeye na kuzinduliwa kwa kundi hilo kulifanya auze album yake ya Noblesse obliges.

mwaka 1994,alipewa tuzo ya  Meilleur na  Africa Music Awards  na kufanikiwa kuliteka soko la kimataifa na kumletea mafanikio makubwa. Na hilo lilimletea tuzo nne za  Kora mnamo mwaka  2001 na tuzo ya  msanii bora wa karne mwaka  2005 katika tuzo za kora  Koffi ni msanii na mwanamuziki mwenye album lukuki katika soko katika Jamhuri yote ya Kidemokrasia ya Congo, hii ndo kazi ya Diego, tazama upishi wake katika Abra Kadabra. twendeeeee

Tuesday, August 14, 2012

Yatokanayo na Olimpics








Wanamichezo watano waliohudhuria michezo ya Olympic jijini London Uingereza kutoka nchini Cameroon, wanasema wanataka ukimbizi kuendelea kubaki nchini Uingereza baada ya kutoweka katika kijiji cha Olympic wiki iliyopita.
Wanamichezo hao wanaume watano wote wakiwa ni mabondia wameiambia BBC kuwa waliondoka katika kijiji cha mashindano ya Olympic mashariki mwa London baada ya kutishiwa na maafisa wa juu wa timu ya Olympic ya Camerron, kuwa wangeadhibiwa iwapo wangeshindwa katika mashindano hayo kwa kuondoka mikono mitupu bila ya kupata medali.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa mabondia hao THOMAS ESSOMBA  amesema wanataka kubaki nchini Uingereza ili kuendeleza taaluma yao ya kimichezo katika ndondi .


                                             Thomas Essomba

 Essomba ameenda  mbali zaidi na kudai kuwa  viongozi wa msafara wao waliwatisha kwa kuanza kuwaamuru wale waliokuwa tayari wameshiriki michezo mingine na kushindwa kusalimisha hati zao za kusafiria.

Monday, August 13, 2012

NUKUU- TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU









                                   FAUSTIN MUSA


                                     SAMSON RAMADHANI


Ndoto za wanamichezo wa Tanzania kurudi nchini na medali toka kwenye michezo ya olimpiki zimefifia baada ya wanariadha FAUSTIN MUSA na SAMSON RAMADHANI kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya marathon yaliyofanyika Jana huko jijini London.
FAUSTIN MUSA alishika nafasi ya 33 huku mwenzie SAMSON RAMADHAN akimaliza kwenye nafasi ya 66 .
Katika mashindano hayo mwanariadha toka UGANDA, STEPHEN KIPROTICH alifanikiwa kutwaa medali ya dhahabu baada ya kumaliza mbio hizo ndani ya muda wa masaa mawili  dakika nane na sekunde moja mbele ya wanariadha toka KENYA, ABEL KIRUI na WILSON KIPROTICH walioshika nafasi ya pili na ya tatu kwa mpangilio.

                    STEPHEN KIPROTICH

Medali aliyotwaa STEPHEN KIPROTICH ndiyo medali pekee ambayo Taifa la UGANDA limeweza kutwaa kwenye michezo ya olimpiki mwaka huu huku Kenya wakiwa wamekusanya jumla ya medali 11  ambapo medali mbili ni za dhahabu , nne za shaba na tano za fedha.