Rwanda imechaguliwa kuwa mwanachama
wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa miaka miwili ijayoKura hiyo
inakuja siku moja baada ya ripoti ya Umoja wa mataifa kufichuliwa ikisema kuwa
nchi hiyo inaunga mkono waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Nchi
zitakazoshikilia nafasi tano zisizo za kudumu katika baraza hilo lenye
wanachama kumi na tano, ziliamuliwa na umoja wa mataifa jana.Argentina, Australia, Korea Kusini
na Luxembourg pia wameteuliwa kuketi kwenye baraza hilo.Kulingana na ripoti hiyo ya
wataalamu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na ambayo ilifichuliwa na
shirika la habari la Reuters, waziri wa ulinzi wa Rwanda anaongoza kw akutoa
amri kwa waasi wa M23 wanaoendeleza uasi Mashariki mwa DRC tangu mwezi Aprili.Wataalamu pia walishutumu Uganda kwa
kuunga mkono waasi.Rwanda na Uganda, zimekanusha madai hayo.







