Wednesday, January 30, 2013

Mnada wa ndege ya Rais Malawi


                                                           Ndege ya Rais wa Malawi!
                              Rais Joyce Banda amekataa kuitumia ndege hiyo kwa usafiri wake
Serikali ya Malawi imewaalika watu wenye nia ya kununua ndege ya rais wa nchi hiyo yenye viti 14.Ndege hiyo inauzwa kama hatua ya rais kupunguza matumizi ya pesa za serikali.Taarifa zinazohusianaAfrikaDuru katika ofisi ya rais Joyce Banda, zinasema kuwa ndege hiyo itauzwa kwa yule atakayeinunua kwa bei ya juu zaidi.

"LULU" ATINGA URAIANI KWA DHAMANA


















Lulu na mama yake, na Dk Cheni, ambaye inasemekana ndiye aliyemuingiza lulu katika tasnia ya filamu!na alikuwepo kushuhudia Lulu akipata dhamana.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KANDA, WA MASHAURIAN​O WA BARAZA LA VIJANA WA JUMUIYA YA MADOLA.

ZAMBIA YAPIGWA KUMBO AFCON


                                   Timu ya kandanda ya taifa ya Zambia, Chipolopolo


Zambia yapigwa kumbo AFCON 2013Timu ya kandanda ya taifa ya Zambia, Chipolopolo, imekuwa mabingwa watetezi wa kwanza kupigwa kumbo kwenye michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwenye mechi za makundi katika kipindi cha miaka 21 iliyopita.

Thursday, January 24, 2013

THE SHOCKING MOMENT £170,000-A-WEEK CHELSEA STAR EDEN HAZARD KICKED A BALLBOY IN THE RIBS

Mambo yameanza!

Lete!

STYLE YA NYWELE YENYE KUKUPA MUONEKANO CHINI YA UMRI WAKO!



Michelle Obama
Kerry Washington

Jinsi mkongwe Serena Williams alivyo tolewa nishai na binti wa miaka 19




Binti wa Kimarekani Sloane Stephens(19) alifanikiwa kusambaratisha mkongwe Serena Williams katika mchezo wa robo fainali wa mashindano ya wazi ya 'Tennis' huko Australia. Kushindwa huko kulimsababisha Serena kuipigiza 'racket' sakafuni na kuiharibu kama ionekanavyo kwenye picha hapo juu.Yasemekana kushindwa kwa Serena kuchangiwa na mauvimivu ya mgongo aliyoyapata katikati ya mchezo na kupelekea Sloane kushinda kwa 3-6, 7-5, 6-4.

 Baada ya mchezo kwisha, Sloane hakuamini kama amefanikiwa kuuangusha mbuyu.Aliongea kwa utani akisema chumbani kwake amebandika picha ya Serena ukutani, sasa ataenda kuitoa na kubandika yake.

Msanii Hussein Machozi aliwahi kupelekwa chumba cha maiti akizaniwa amekufa





                                                                      Hussein Machozi
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hussein Machozi ameelezea kisa cha kudhaniwa amekufa kupitia Clouds FM alipokua akifanyiwa interview. Alijeruhiwa akiwa uwanjani akicheza mpira na kupoteza fahamu  kisha akakimbizwa hospitali ambapo alifanyiwa vipimo vyote na kuonekana amefariki. Alipelekwa Chumba cha kuhifadhia maiti. Muuguzi wa zamu alipokua akitaka kwenda kumchoma sindano ili asiharibike alikurupuka.

Hali ya afya ya Msanii Matumaini siyo nzuri



                                                             Matumaini


HALI ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini si ya kuridhisha kutokana na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini MsumbijiKutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishio Msumbiji wamejitolea kumchangia nauli ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa ndugu zake

VIDEO: Ofisa wa TRA Arusha akichukua rushwa waziwazi




Video hii imerekodiwa kutoka kwenye simu ya mkononi na inamuonyesha Ofisa wa TRA Arusha akipokea rushwa toka kwa mteja ili aweze kumhudumia.
Ofisa huyu yupo mapokezi (reception) na inadaiwa ni kawaida yake kupokea Rushwa na kuwa usipompa anadai kwa nguvu.Wafanyakazi wa TRA na wakubwa zake inadaiwa wanajua kinachoendelea lakini hawachukui hatua..
Kuna utendaji mbovu, lugha chafu kwa wateja na za majivuno na mambo mengi yanayofanana na hayo.
Mamlaka husika zinaombwa kuingilia kati TRA Mapato, (karibu na Benki Kuu tawi la Arusha) ili raia wapate huduma bila vikwazo vya rushwa toka kwa maofisa kama huyu.
Chanzo:fikrapevu.com

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATOA MAONI KWA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA MPYA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Sinde Warioba, wakati tume hiyo ilipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuchukua maoni yake binafsi ikiwa ni sehemu ya kuchangia maoni ya katiba mpya. 

Tuesday, January 8, 2013

WALIOFAULU DARASA LA SABA 2012 KWENDA KAWE UKWAMANI WARIPOTI SHULENI LEO




Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kawe Ukwamani, jijini Dar es Salaa, Peter John (wa nne kushoto mwenye suruali) akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi walioripoti shuleni hapo leo asubuhi kwa ajili ya kuanza muhula wa masomo ya Sekondari baada ya kufalu mtihani wa darasa la saba wa 2012 na kuchaguliwa kujiunga na shule hiyo. Wanafunzi wote waliochanguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari Kidacho cha kwanza, na wale wa sekondari waliokuwa mapumzikoni, wametakiwa kuripoti shuleni hii leo kote nchini.

Brent Musburger, 73, livens up the first half of BCS title game with comments on AJ McCarron’s girlfriend





Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea! Ni kawaida kuona familia ya mchezaji ikienda yote uwanjani kumpa saport ndugu yao! Timu yake ikishinda wanafurahi pamoja naye lakini ikiwa vinginezo wanahuzunika pamoja naye na kurudi home vichwa chini!

Washukiwa wa mapenzi ya jinsia moja waachiliwa huru


                                                Wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja

Mahakama moja ya rufaa nchini Cameroon, imefutilia mbali hukumu dhidi ya watu wawili waliofungwa jela mwaka wa 2011, baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
 Wakili  wa wawili hao,  Alice Nkom , amesema amefurahishwa na uamuzi huo kwa sababu jaji aliyetoa hukumu dhidi yao, alifanya hivyo chini ya shinikizo ya watu fulani.Novemba mwaka wa 2011, mahakama iliwapata na hatia wawili hao na kuwahukumu kifungo cha miaka mitano gerezani, baada ya polisi kuwakamata wakifanya ngono katika gari moja mjini Yaunde.

Messi ashinda tuzo ya Ballon d'Or



                                                     Lionell Messi

Mshambulizi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa nne mfululizo.

Tapeli anaswa kwa kuiba mamilioni ya dola


                                Hamza Bendelladj baada ya kukamatwa na polisi mjini Bengkok

Mshukiwa mmoja wa udakuzi wa komputa ambaye anasakwa na idara ya ujasusi nchini Marekani, FBI, kuhusiana na madai ya kuiba mamilioni ya madola kutoka benki za Marekani, ili kufadhili maisha ya anasa, amekamatwa mjini Bangkok Thailand.
Shirika hilo la FBI, limekuwa likimsaka mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24, Hamza Bendelladj, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya komputa, kutoka Algreia kwa zaidi ya miaka mitatu.

Friday, January 4, 2013

Fahamu madhara ya kuongeza makalio



VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni imewashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya madawa hayo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa madawa hayo badala ya kumfanya mwanamke awe laini, video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka wa makalio pamoja na kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu za nyuma (chini) baada ya muda mfupi.

Mvua: Mamia wakwama, wawili wafariki Singida


Wananchi wakivuka kwa miguu katika Daraja la Manung’una, lililopo katika Kijiji cha Msisi, Singida ambalo limekatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.



Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa waliofariki dunia kutokana na mvua hizo ni Xue Hui (36), maarufu kwa jina la Kevin na Mariamu Samweli (18), mkazi wa Kijiji cha Maluga ambao walifariki dunia kwa nyakati tofauti baada ya kusombwa na maji.

Mancini agombana na Balotelli



                                              Mancini akimvuta shati Baloteli

Mshambulizi wa Manchester City Mario Balotelli amezozana na kocha wake Roberto Mancini wakati walipokuwa mazoezini.

Mechi ya AC Millan yasitishwa kutokana na Ubaguzi wa rangi




                                   Prince Boateng


Mchezo wa kirafiki kati ya timu ya AC Milan na Pro Patria za nchini Italia, Ulisitishwa na ya wachezaji kutoka nje ya uwanja kwa sababu ya kutolewa maneno ya ubaguzi dhidi ya wachezaji weusi.Mchezaji wa AC Milan Kevin-Prince Boateng alibeba mpira dakika ya 25 ya mchezo na kuupiga kuelekea walikokaa watazamaji.

TUKUTUKU YAZUA JAMBO NCHINI INDONESIA


                                     PIKIPIKI ALMAARUFU KAMA BODABODA.



Meya wa LUKSA OMAWE,  Nchini Indonesia , bwana SAUDI YAHYA amesema Wanawake kukaa kwa kuangalia mbele ni ukiukwaji wa maadili ya kiislamu na kuamuru wakae upande.

Thursday, January 3, 2013

PICHA MBALIMBALI ZA SAJUKI ENZI ZA UHAI WAKE



RIP SAIDI  KILOWOKO A.K.A SAJUKI!
Sajuki alipendana mno na mkewe WASTARA!

WANWAKE WA AFRICA 11 BORA KATIKA SIASA 2012



2012 uliwaendea vyema wanawake wanasiasa barani Africa, wanawake 11, miongoni mwao ni marais 2 na 1 ni kiongozi katika umoja wa Africa , nakupeleka uwatambue na huu ni utafiti uliofanywa katika bara hili kutambua mchango wa wana siasa hao katika siasa za Africa.!
                                                 Charity Ngilu Mbunge katika bunge la Kenya.

Elsie Kanza Mkurugenzi na kiongozi kutoka katika nchi za  Africa katika  World Economic Forum -  akitokea Tanzania