Matumaini
HALI ya msanii wa
maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini si ya kuridhisha kutokana
na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini MsumbijiKutokana na hali yake ya kiafya
kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishio Msumbiji wamejitolea kumchangia nauli
ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa
ndugu zake
Akizungumza jijini Dar
es Salaam mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni , Kaftany
Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa wa msanii huyo ingawa
haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka sasaAlisema kutokana na hali
kuwa mbaya baadhi ya watanzania wameamua kumchangia msanii huyo ili aweze
kurejea nyumbani ili taratibu za matibabu zifwatwe
"Ni kweli hali ya
msanii mwenzetu si nzuri anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na
Dokta hivyo bado hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na juhudi
zinazofanywa ili kumrudisha nyumbani " alisema MasoudAliongezea kuwa kwa
upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedha kwa ajili ya
matibabu ya msanii huyo atakapofika hapa nchini
Matumaini ni msanii
kwenye upande wa uchekeshaji.alianza kazi hiyo katika kundi la Kaole na
kujipatia umaarufu kwa kuigiza na msanii mwenzie KiweweChanzo:
audifacejackson.blogspot.com
No comments:
Post a Comment