Mshambulizi
wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameshinda tuzo ya
Ballon d'Or kwa mwaka wa nne mfululizo.
Abby
Wambach, alishinda tuzo kwa upande wa kina dada naye Vicente del Bosque,
akituzwa kuwa kocha bora.Timu bora ya kwana ilijumuisha wachezaji wanaoshiriki
katika ligi ya Uhispania pekee.
Messi
alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya the Ballon d'Or, tuzo ambayo hukabithiwa
mchezaji bora wa mwaka katika sherehe iliyofanyika mjini Zurich
Messi
alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioteuliwa na jopo la wandishi wa
habari na makocha wa timu za taifa, manaodha wa timu hiyo wakiwa ni pamoja na
Iniesta na Ronaldo.
Mesi sasa ni
mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo ya Ballons d'Or, kwa miaka minne
mfululizo, rekodi anayoshikilia na aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa na rais wa
UEFA kwa sasa Michel Platini.
Kikosi cha wachezaji bora wa mwaka
2012
•Iker Casillas
(Real Madrid)
•Dani Alves
(Barcelona)
•Gerard
Pique (Barcelona)
•Sergio
Ramos (Real Madrid)
•Marcelo
(Real Madrid)
•Andres
Iniesta (Barcelona)
•Xabi Alonso
(Real Madrid)
•Xavi
(Barcelona)
•Cristiano
Ronaldo (Real Madrid)
•Radamel
Falcao (Atletico Madrid)
•Lionel
Messi (Barcelona)
No comments:
Post a Comment