Prince
Boateng
Mchezo wa kirafiki kati ya timu ya AC Milan na Pro Patria za
nchini Italia, Ulisitishwa na ya wachezaji kutoka nje ya uwanja kwa sababu ya
kutolewa maneno ya ubaguzi dhidi ya wachezaji weusi.Mchezaji wa AC Milan
Kevin-Prince Boateng alibeba mpira dakika ya 25 ya mchezo na kuupiga kuelekea
walikokaa watazamaji.
Boateng mchezaji wa kimataifa wa Ghana baadaye alivua jezi
yake na kufuatwa na wachezaji wenzake wa timu zote mbili, na maafisa waliokuwa
katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Pro Patria.Kumekuwa na kauli
zilizotolewa zikiwataka mashabiki wa wachezaji kuacha kutumia lugha ya ubaguzi.
Akiwa anatoka uwanjani, Boateng aliwapongeza watazamaji
waliokabiliana na vitendo vya ubaguzi vilivyoonyeshwa na baadhi ya mashabiki.Baadaye
ikafahamika kuwa mechi hiyo isingeendelea na tovuti rasmi ya AC Milan imesema
wachezaji wengine weusi wa timu hiyo akiwemo M'Baye Niang, Urby Emanuelson na
Sulley Muntari - walikabiliwa na vitendo vya ubaguzi uwanjani.
Koocha wa AC Milan, Massimiliano Allegri amewambia waandishi
wa habari: "Tumesikitishwa na kuhuzunishwa kwa kile kilichotokea.Mkurugenzi
wa uratibu wa AC Milan Umberto Gandini ameiambia BBC Sport: "inasikitisha
sana lakini tulitakiwa kuonyesha ishara kali. Tumefurahishwa sana na uamuzi wa
wachezaji wote wa Milan wa kutoka nje ya uwanja."
Wachezaji wenzao , akiwemo nahodha wa Manchester City
Vincent Kompany, wamemuunga mkono Boateng na wachezaji wenzake kwa uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment