Video hii imerekodiwa
kutoka kwenye simu ya mkononi na inamuonyesha Ofisa wa TRA Arusha akipokea
rushwa toka kwa mteja ili aweze kumhudumia.
Ofisa huyu yupo
mapokezi (reception) na inadaiwa ni kawaida yake kupokea Rushwa na kuwa
usipompa anadai kwa nguvu.Wafanyakazi wa TRA na wakubwa zake inadaiwa wanajua
kinachoendelea lakini hawachukui hatua..
Kuna utendaji mbovu,
lugha chafu kwa wateja na za majivuno na mambo mengi yanayofanana na hayo.
Mamlaka husika
zinaombwa kuingilia kati TRA Mapato, (karibu na Benki Kuu tawi la Arusha) ili
raia wapate huduma bila vikwazo vya rushwa toka kwa maofisa kama huyu.
Chanzo:fikrapevu.com
No comments:
Post a Comment