Wananchi wakivuka kwa miguu katika Daraja la Manung’una, lililopo katika Kijiji cha Msisi, Singida ambalo limekatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Habari
zilizopatikana jana zimeeleza kuwa waliofariki dunia kutokana na mvua hizo ni
Xue Hui (36), maarufu kwa jina la Kevin na Mariamu Samweli (18), mkazi wa
Kijiji cha Maluga ambao walifariki dunia kwa nyakati tofauti baada ya kusombwa
na maji.
MVUA zinazoendelea
kunyesha mkoani Singida, zimesababisha maafa makubwa baada ya watu wawili,
mmoja akiwa raia ya China, kufariki dunia kwa kusombwa na maji, huku mamia ya
abiria wakikwama njiani baada ya daraja linalounganisha mkoa huo na mingine
kukatika.
Kukatika kwa Daraja la
Munung’una kwa siku mbili sasa, kumesababisha msongamano mkubwa wa magari
yanayokadiriwa kuwa zaidi ya 300.
Habari zilizopatikana jana
zimeeleza kuwa waliofariki dunia kutokana na mvua hizo ni Xue Hui (36), maarufu
kwa jina la Kevin na Mariamu Samweli (18), mkazi wa Kijiji cha Maluga ambao
walifariki dunia kwa nyakati tofauti baada ya kusombwa na maji.
Vifo vyao vimeongeza
idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mvua mkoani Singida kufikia sita
katika siku tatu zilizopita. Mvua za juzi, zilisababisha watu wanne wa familia
moja katika Wilaya ya Mkalama kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba ya
tembe.
Mkuu wa Wilaya hiyo,
Edward Ole Lenga alisema raia huyo wa China, alifariki dunia juzi jioni katika
Kijiji cha Gumanga Wilaya ya Mkalama baada ya gari alilokuwa anasafiria
kusombwa na maji... “Mchina huo alikuwa na mtoto wake ambaye alinusurika kifo.”
Alisema Mariamu alifariki dunia baada ya kusombwa na maji katika Mto Kiula uliopo katika Kijiji cha Igonia. “Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida.”
Alisema Mariamu alifariki dunia baada ya kusombwa na maji katika Mto Kiula uliopo katika Kijiji cha Igonia. “Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida.”
Abiria
wakwama
Mvua hizo kubwa zilizonyesha tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, zilisababisha daraja hilo la Munung’una lililopo katika Kijiji cha Msisi wilayani Singida kuvunjika.
Kutokana na athari hiyo, kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari baada ya mawasiliano kati ya Singida na mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani kukatika.
Mvua hizo kubwa zilizonyesha tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, zilisababisha daraja hilo la Munung’una lililopo katika Kijiji cha Msisi wilayani Singida kuvunjika.
Kutokana na athari hiyo, kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari baada ya mawasiliano kati ya Singida na mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani kukatika.
Baadhi ya wananchi
walilalamikia uharibifu huo wakisema umetokana na ujenzi wa daraja hilo kuwa wa
kiwango cha chini. Dereva, George Medadi akitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam,
alisema daraja hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujengwa chini ya kiwango.
Dereva mwingine, Iddi
Mussa alisema barabara nyingi zinazojengwa zimekuwa hazisimamiwi ipasavyo,
kitendo kinachochangia kuharibika haraka na kuisababishia Serikali hasara
kubwa.
Meneja wa Wakala wa
Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Singida, Mhandisi Yustaki Kangole alisema
wamekubaliana na Kampuni ya Ujenzi ya Chico kutoka China ambayo ndiyo
iliyojenga barabara hiyo kufukia shimo lililokata daraja hilo kwa vifusi vya
mawe makubwa ili iendelee kutumika mapema iwezekanavyo.
“Kwa sasa tunafanya kazi
hii ya muda na baada ya eneo hili kukauka, ndipo ukarabati mkubwa utafanywa ili
kuimarisha barabara hii muhimu kwa uchumi wa taifa,” alisema.
Mhandisi Kangole alisema
Chico ilijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami na kuikabidhi kwa Serikali
mwaka 2008.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi
alisema kutokana na eneo hilo kufurika watu na mali, wameimarisha ulinzi na
kufungua kituo kidogo cha kutolea huduma za afya na kudhibiti uwezekano wa
kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.
No comments:
Post a Comment