Binti wa
Kimarekani Sloane Stephens(19) alifanikiwa kusambaratisha mkongwe Serena
Williams katika mchezo wa robo fainali wa mashindano ya wazi ya 'Tennis' huko
Australia. Kushindwa huko kulimsababisha Serena kuipigiza 'racket' sakafuni na
kuiharibu kama ionekanavyo kwenye picha hapo juu.Yasemekana kushindwa kwa
Serena kuchangiwa na mauvimivu ya mgongo aliyoyapata katikati ya mchezo na
kupelekea Sloane kushinda kwa 3-6, 7-5, 6-4.
Baada ya mchezo kwisha, Sloane hakuamini kama
amefanikiwa kuuangusha mbuyu.Aliongea kwa utani akisema chumbani kwake
amebandika picha ya Serena ukutani, sasa ataenda kuitoa na kubandika yake.
No comments:
Post a Comment