Mahakama moja ya rufaa nchini Cameroon, imefutilia mbali
hukumu dhidi ya watu wawili waliofungwa jela mwaka wa 2011, baada ya kupatikana
na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wakili wa wawili hao,
Alice Nkom , amesema amefurahishwa na
uamuzi huo kwa sababu jaji aliyetoa hukumu dhidi yao, alifanya hivyo chini ya
shinikizo ya watu fulani.Novemba mwaka wa 2011, mahakama iliwapata na hatia
wawili hao na kuwahukumu kifungo cha miaka mitano gerezani, baada ya polisi
kuwakamata wakifanya ngono katika gari moja mjini Yaunde.
Wawili hao walikana mashtaka hayo.Lakini mapema hii leo
mahakama hiyo ya rufaa iliagiza kuwa washukiwa hao hawakuwa na kosa lolote.Akizungumza
na BBC Bi Nkom alisema kuwa uamuzi huo sio wa kushangaza.
''Wateja wangu hawakuwa wakifanya lolote wakati
walipokamatwa na polisi'' Alisema Bi Nkom.Kwa kuwa walikuwa wamevalia nguo za
wanawake na kujipaka vipodozi, polisi walisema kuwa wao ni wanachama wa mtandao
mmoja unaohimiza mapenzi ya jinsia moja''
Hata hivyo amesema, upande wa mashtaka haujaelezea ikiwa
utawasilisha rufaa kupinga uamuzi huo wa mahakama ya juu zaidi.Wanaume hao
wawili wanatarajiwa kuachiliwa siku ya Jumanne LEO.
Shirika la kimataifa linalotetea maslahi ya wapenzi wa
jinsia moja, limepongeza uamuzi huo.Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Andre
Banks, amesema ni dhihirisho kuwa mahakama zinaweza kutekeleza majukumu yake
kwa njia ya haki na usawa.
Bi Nkom, vile vile ameiambia BBC kuwa mwezi uliopita,
mahakama hiyo ya rufaa, iliidhinisha hukumu ya kifungo cha miaka mitatu
gerezani dhidi ya raia mwingine wa Cameroon, Roger Jean-Claude Mbede, chini ya
sheria za kupambana na mapenzi ya jinsia moja.
mwenye miwani ndiye Roger Jean-Claude Mbede akiwa kwenye interview na mwandishi habari.
No comments:
Post a Comment