Timu ya kandanda ya taifa ya Zambia, Chipolopolo
Zambia yapigwa kumbo AFCON 2013Timu ya kandanda ya taifa ya
Zambia, Chipolopolo, imekuwa mabingwa watetezi wa kwanza kupigwa kumbo kwenye
michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwenye mechi za makundi katika
kipindi cha miaka 21 iliyopita.
Zambia ilitoka sare tasa jana dhidi ya Burkina Faso, ambayo
imefuzu kuingia robo fainali ya mashindano ya mwaka huu, AFCON 2013, kwenye
mechi iliyochezwa katika uwanja wa Mbombela nchini Afrika Kusini. Sare ya tatu
kwa Chipolopolo haikutosha kuiwezesha kusonga mbele katika mashindano hayo.
Timu ya mwisho iliyoshinda kombe la mataifa ya Afrika na
kushindwa kusonga mbele katika duru ya pili kwenye mashindano yaliyofuata ni
Algeria mnamo mwaka 1992.
Wachezaji wa Burkina
Faso Burkina Faso imeongoza katika kundi C na kuweka historia yake, huku
ikifuzu kwa raundi ya pili kwa mara ya kwanza katika nchi ya kigeni. Burkina
Faso imewahi kusonga mbele katika mashindano ya kuwania kombe la mataifa
Afrika, mara moja tu wakati ilipoyaandaa mnamo mwaka 1998.
Kocha wa Burkina Faso, raia wa Ubelgiji, Paul Put, amesema
anadhani huu ni ufanisi mkubwa kabisa wa timu ya nchi hiyo kwa kuwa iliwahi
kuyaandaa mashindano hayo mara moja na ikafaulu kufika nusu fainali. "Lengo
letu la kwanza tulitaka kufanya vyema zaidi kuliko mashindano ya hivi karibuni
ya kombe la mataifa ya Afrika na tulikuwa tumefanikiwa kwa kutoka sare dhidi ya
Nigeria na Ethiopia. Nadhani ni historia kwa Burkina Faso," akaongeza
kusema kocha Put.
Zambia
haikung'ara
Kocha wa Zambia, Herve Renard, amebakia kuwa mwingi wa
matumaini na mwanafalsafa. "Ni bora uwe umeshinda kitu katika maisha yako,
kuliko kuingia robo fainali kila mara lakini usifaulu kushinda chochote,"
amesema kocha huyo na kuongeza kusema, "Huu sio mwisho wa dunia. Zamani
tulikuwa tukirudi nyumbani mara nyingi baada ya raundi ya kwanza, na leo lazima
tukubali kwamba huu ni mchezo wa soka."
Kocha wa Zambia, Herve Renard
Kocha wa Zambia, Herve Renard Zambia haikuonyesha mchezo
mzuri na mshambuliaji wake matata, Collins Mbesuma, alikosa nafasi kadhaa za
kuutikisa wavu wa Burkina Faso. Kwa upande wao Burkina Faso walifahamu
walihitaji sare tu kuweza kufuzu na waliridhika kucheza katikati mwa uwanja ili
kupunguza kasi ya mchezo huo, hususan baada ya kumpoteza kipa wao mahiri, Alain
Traore, kutokana na jeraha alilolipata dakika ya 10 ya mtanange huo."Viungo
vya leo ilikuwa ni pilipili nyingi na chumvi kidogo kwenye mchuzi," ndivyo
alivyotamka kocha wa Burkina Faso, Paul Put.
Zambia ilipata changamoto kubwa kutokana na hali ya uwanja
wa Mbombela kuwa na mchanga mwingi. Kocha wa Chipolopolo, Renard, amesema,
"Nikiulaumu uwanja basi watu watasema nalia, lakini nadhani baada ya
mkutano huu na waandishi wa habari unahitaji tu kwenda uwanjani na ujionee kama
inawezekana kucheza kandanda safi."
Nigeria
yaitwanga Ethiopia
Kwenye mechi nyengine ya kundi C, Nigeria iliinyoa Ethiopia
bila maji kwa kuitandika mabao 2-0 katika uwanja wa mjini Rustenburg. Kocha wa
Nigeria, Stephen Keshi, amesema, "Ushindi huu ni wa Wanigeria wote popote
walipo ulimwenguni. Huu ni wakati wa kushangilia."
Ethiopia ikichuana na Nigeria
Ethiopia ikichuana na
Nigeria Ushindi wa Nigeria dhidi ya Ethiopia umewatia tumbo joto wachezaji huku
wakisubiri kuvaana na Cote d'Ivoire kwenye robo fainali. Burkina Faso inasubiri
kukwaana na mshindi wa mechi ya kundi C kati ya Togo na Tunisia mjini Nelsprut
itakayochezwa baadaye leo. Ethiopia na Zambia wanafunganya virago na kuelekea
uwanja wa ndege tayari kurejea nyumbani.
No comments:
Post a Comment