Ndege ya Rais wa Malawi!
Serikali ya
Malawi imewaalika watu wenye nia ya kununua ndege ya rais wa nchi hiyo yenye
viti 14.Ndege hiyo
inauzwa kama hatua ya rais kupunguza matumizi ya pesa za serikali.Taarifa
zinazohusianaAfrikaDuru katika ofisi ya rais Joyce Banda, zinasema kuwa ndege
hiyo itauzwa kwa yule atakayeinunua kwa bei ya juu zaidi.
Mtangulizi
wake, hayati Rais Bingu wa Mutharika, alikashifiwa vikali kwa kununua ndege
hiyo miaka mitano iliyopita kwa takriban dola milioni 8.9
Wahisani
walisitisha msaada wa dola milioni nne nukta nne kwa Malawi punde baada ya
serikali ya Mutharika kuinunua ndege hiyo.
Bi Banda
amekataa kusafiri kwa ndege hiyo, tangu kuchukua hatamu za uongozi mwezi Aprili
mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Mutharika.
'Nafuu
kutumia'Alisema kuwa pesa zitakazopatikana baada ya kuiza ndege hiyo kuuzwa ,
zitatumiwa kutoa huduma muhimu kwa watu maskini wa Malawi.
Duru
zilisema kuwa ndege hiyo iko katika hali nzuri kuweza kutumiwa, na inaweza
kupaa kwa kilomita 8,380 bila kusimama.Mnada utakuwa wazi kwa yeyote atayetaka
kuinunua
Wakati
Mutharika alipoinunua ndege hiyo, alisema haitaigharimu serikali pesa nyingi
kuitumia.Ingawa baadaye upinzani pamoja na wahisani walimtuhumu kwa kutumia
vibaya pesa za serikali.
Malawi ni
mojawapo ya nchi maskini sana barani Afrika.Ilikumbwa na maandamano juu ya
kupanda kwa bei ya maisha rais Mutharika alipokuwa anakamilisha muhula wake wa
utawala.Tangu
kuitawala nchi hiyo, Bi Banda amechukua hatua kadhaa za kurejesha uhusiano
mzuri na wahisani.
No comments:
Post a Comment